Eei nilikuwa nimalizie Xmass ndio niibuke tena hapa JF ,lakini ulipangalo silo alilokuekea Mwenyezi Mungu,ni baada ya kusikia Zanzibar imetoa kipigo cha paka mwizi.
Yaani huku kwetu tunamsemo unasema kupuruzia na pale mwanzo tuliwapuruzia angalau mpate kuvuka na hamkuwa na fadhila ,maana kumbe hata nchi mnayowakilisha haipo ,sielewi mmetokea nchi gani ,yaani mmeingia katika mashindano ya watu kinyemelanyemela na kutaka kujifanya mnajua kucheza kuliko watu wenye nchi zao.
Sasa hata ushindi wa tatu mmeukosa na mnarudi mlikotoka sijui mmetoka wapi.Nasikia ni kutoka Tanzania ila nijuavyo Tanzania ni Muungano wa nchi mbili moja ikiwa ipo na ingine imefulia tokea miaka ya sitiini.
Hivyo ile haki ya nyie kushiriki katika kombe hilo hamna kabisa na ushindi mliopata ungeweza hata kukatiwa rufaa ,isipokuwa huruma tu ndio zimewakumba kama waliotoka kwenye mafuriko.
Mara ingine msishiriki katika mashindano ya watu wenye nchi zao ambazo zipo hai na zitaendelea kuwepo.Kwanza ni aibu kushiriki mnadusa katika mambo ambayo nyie hayawahusu.
Zanzibar imetoa somo kubwa sana na itabidi kwanza mujiulize Zanzibar imeifunga nchi gani ? Ndio muweze kujibu hii hoja kama haitoshi muulizeni Pinda hivi nyie mukiwakilisha nchi gani na katika kugombea mshindi wa tatu ni nchi gani iliwafunga ,Je hii ni nchi ? Mbona imetufunga nje ya mipaka ya Tanzania na wewe ulisema si nchi nje ya mipaka ? Lazima atakwambieni Kikwete ndie aliesema hivyo.
heheheheeeeeeeeeeeee
nimefurahi sana na kijembe hiki kinachoakisi uzito wa baadhi ya akili kuelewa mambo!
kwa kukusaidia mkuu, sio nchi zilizoshindana na kama zingekuwa nchi, zanziba isingeruhusiwa kushiriki. zilizoshingana ni timu zinazoidhinishwa na
vyama wanachama wa cecafa!
muhidini ndolanga alikuwa mwerevu sana wa mambo ya soka ndoio maana akina kapuya na uprofesa wao walichemsha. walikuwa na akili kama hizi wakifikiri fat ilikuwa idara ya serikali umbe kilikuwa chama kilichundwa na wadau, kikiwa huru na kwa uhuru kiliomba uanachama katika chama kingine huru cha fifa na kukubaliwa hivyo serikali haina uhalali wa kuingilia mambo ya soka kama serikali, bali inaweza kushauri tu kama wadau wengine.
sasa wewe mzenji, ni kuwa zanziba si nchi, ilijinyonga yenyewe tangu 1964, hiyo ilyoshiriki mashindano si timu ya taiifa ni timu ya
mkoa wenye uanachama wa cecafa! kuhusu kushinda ama kutoshinda, siku zote ni
dakika 90 ndizo huamua! hujasikia mabingwa wa ligi kuu ya
nchi ya tz yanga imefungwa na timu ya daraja la kwanza tmk united? hiyo ndo soka, hakuna cha ajabu.
asiyekubali kushindwa si mshindani,
hongereni sana wakubwaaaaaaaaa kwa ushindi ila mtuombee tuepushwe na mwalmu wa nidhamu(discipline master) wa timu yetu, maximo. mtuombee angalau nasi tupate mwalimu wa mpira hata kama ni mzawa. maximo alituzuga kuwa amekuja kufundisha mpira, kumbe amekuja kufundisha nidhamu! na jk anavyomtetea, nadhani naye ameishakuwa mwanamtandao!!!!!!!!
Mungu ibariki tanzania