Kombe la Dunia 2026: Afrika kuipa support Mexico leo ni zao la Xenophobia?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Leo ndio ile siku! Kipenga cha ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026 kinapulizwa, lakini huku mitandaoni mambo yamegeuka. Badala ya bara la Afrika kusimama nyuma ya Afrika Kusini (Bafana Bafana), Waafrika wameamua kuhamia Mexico jumla jumla! Mtandaoni kumechafuka haswa!

images - 2026-06-11T142048.874.jpeg
Ukiingia Facebook na X (Twitter), kurasa za timu kubwa kama Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates zimefurika "hasira za kisasi." Sababu? Kumbukumbu chungu za Xenophobia.

Screenshot_20260611_142651_TikTok Lite.jpg
Waafrika wameamua kuwalipizia watoto wa madiba kisaikolojia, na silaha yao kuu ni kubadili majina kuwa vijana kutoka Mexico.

images - 2026-06-11T142116.855.jpeg
Kuanzia Lusaka mpaka Bujumbura, Accra hadi Dar es Salaam, Lagos mpaka Nairobi majina yamebadilika fasta. Utakutana na maoni kama:

Screenshot_20260611_142927_TikTok Lite.jpg
"Kazi ya kuwapa moyo ni kazi yao Waafrika Kusini sio kazi ya raia wa nchi nyingine, hawachelewi hawa kusema kuwa tumechukua kazi yao ya kuwapa moyo Bafana Bafana, kwanini tuwe wapole wakati walitufukuza?"

Screenshot_20260611_142831_TikTok Lite.jpg
Ndani ya masaa 48 Algorithm za mitandao ya kijamii inapitia magumu sana kwani kuna wengine wanatoa na matusi humo humo, nchi kama Nigeria, Ghana pamoja na Kenya* wameonesha kuwa mstari wa mbele kabsa.

Screenshot_20260611_143057_TikTok Lite.jpg
Mimi ni mzaliwa wa Chato lakini kwa sasa naitwa Alejandro Martines Pablo De la Cruz, tuko nyuma yenu Mexico! 🇲🇽"

images - 2026-06-11T142138.481.jpeg
Ukipita mitandaoni kuna contents nyingi sana za kuwavunja moyo Bafana Bafana, ni kama vile watu wanatema sumu zao bila kuonesha huruma.

hq720 (2).jpg
"Mexico ni ndugu zetu kabsa, hawajawahi kutufukuza wala kutuzuia siku yoyote tukiwa tunaelekea Marekani. Kwa siku ya leo naitwa Francesco Gustavo Hernandez, tuko nyuma yenu Mexico! 🇲🇽"

images - 2026-06-11T142116.855.jpeg
Wengine wameenda mbali zaidi na kujiita Don Carlos, Juanita Josè, na Mateo Alfredo. Leo ni mwendo wa Señor na Señorita!

images - 2026-06-11T142048.874.jpeg
Kama kuna wachezaji wa Bafana Bafana wataingia mtandaoni basi wawe na mtaalamu wa saikolojia aliye vizuri tofauti na hivyo comment section itakwenda kumaliza morali ya wachezaji.

images - 2026-06-11T142138.481.jpeg
Matunda ya Xenophobia ndio haya, haina afya wala utimamu kuendelea kumpenda mtu ambaye kakutimua kwake tena akionesha hasira na jeuri kali sana. Leo wachezaji wa Mexico wanapata support ya ajabu sana.
 
Labda wangeenda kushangilia huko
 
Nina wazo la biashara ambayo nikipata kiasi cha shilling laki tano basi naweza fanya maajabu ukabaki unashangaa..

Jaribu sasa bahati yako..
 
Leo ndio ile siku! Kipenga cha ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026 kinapulizwa, lakini huku mitandaoni mambo yamegeuka. Badala ya bara la Afrika kusimama nyuma ya Afrika Kusini (Bafana Bafana), Waafrika wameamua kuhamia Mexico jumla jumla! Mtandaoni kumechafuka haswa!

Ukiingia Facebook na X (Twitter), kurasa za timu kubwa kama Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates zimefurika "hasira za kisasi." Sababu? Kumbukumbu chungu za Xenophobia.

Waafrika wameamua kuwalipizia watoto wa madiba kisaikolojia, na silaha yao kuu ni kubadili majina kuwa vijana kutoka Mexico.

Kuanzia Lusaka mpaka Bujumbura, Accra hadi Dar es Salaam, Lagos mpaka Nairobi majina yamebadilika fasta. Utakutana na maoni kama:

"Kazi ya kuwapa moyo ni kazi yao Waafrika Kusini sio kazi ya raia wa nchi nyingine, hawachelewi hawa kusema kuwa tumechukua kazi yao ya kuwapa moyo Bafana Bafana, kwanini tuwe wapole wakati walitufukuza?"
Ndani ya masaa 48 Algorithm za mitandao ya kijamii inapitia magumu sana kwani kuna wengine wanatoa na matusi humo humo, nchi kama Nigeria, Ghana pamoja na Kenya* wameonesha kuwa mstari wa mbele kabsa.

Mimi ni mzaliwa wa Chato lakini kwa sasa naitwa Alejandro Martines Pablo De la Cruz, tuko nyuma yenu Mexico! 🇲🇽"
Ukipita mitandaoni kuna contents nyingi sana za kuwavunja moyo Bafana Bafana, ni kama vile watu wanatema sumu zao bila kuonesha huruma.

"Mexico ni ndugu zetu kabsa, hawajawahi kutufukuza wala kutuzuia siku yoyote tukiwa tunaelekea Marekani. Kwa siku ya leo naitwa Francesco Gustavo Hernandez, tuko nyuma yenu Mexico! 🇲🇽"
Wengine wameenda mbali zaidi na kujiita Don Carlos, Juanita Josè, na Mateo Alfredo. Leo ni mwendo wa Señor na Señorita!

Kama kuna wachezaji wa Bafana Bafana wataingia mtandaoni basi wawe na mtaalamu wa saikolojia aliye vizuri tofauti na hivyo comment section itakwenda kumaliza morali ya wachezaji.

Matunda ya Xenophobia ndio haya, haina afya wala utimamu kuendelea kumpenda mtu ambaye kakutimua kwake tena akionesha hasira na jeuri kali sana. Leo wachezaji wa Mexico wanapata support ya ajabu sana.
Tuliwapigania,tukawahifadhi,Leo wanatufukuza,Wacha waonje matunda ya ubaguzi Kwa waafrika wenzao!
 
Back
Top Bottom