Kombe la Dunia kwa Ngazi ya Vilabu kuanza mwaka 2025

Kombe la Dunia kwa Ngazi ya Vilabu kuanza mwaka 2025

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
OFFICIAL: Rais wa Shirikisho la soka Duniani FIFA Bwana Gianni Infantino amethibitisha kuwa mfumo mpya wa Kombe la Dunia kwa upande wa vilabu utaanza mwaka 2025.

Mfumo huo utakuwa na timu 32 na utaendeshwa kama Kombe la Dunia la ngazi ya timu za Taifa.

Umepokeaje?

#FIFAWorldCup
 
Yaani kwenye upande wa vilabu Africa hapo tunaenda kuumbuka sidhani kama wamefikiria vizuri kwenye hilo maana wachezaji wa ulaya na Africa ni mbingu na ardhi kwenye ubora kwenye world hata hao Morocco na Senegal wachezaji wao wengi wanacheza ulaya sasa hapo hakuna usawa ngoja tusubiri.
 
Dah aisee hawa wakuu wa falme ya giza hawataki tuache kubet kbs wakitoa formula hii wanatuwekea nyingine..ni vzr lakini kwa wapenzi wa soka ila kwanini iwe 32..si bora ingekuwa mabingwa wote wa mataifa yao wacheze
Mataifa yako zaidi ya 150, kwa hiyo ukusanye vilabu zaidi ya 150? Hiyo itakuwa bonanza. Mbaya zaidi mataifa mengi yako hovyo kisoka na raha ya mashindano ni kuona ushindani na sio kuona Arsenal 20-Yanga 0.
 
Dah aisee hawa wakuu wa falme ya giza hawataki tuache kubet kbs wakitoa formula hii wanatuwekea nyingine..ni vzr lakini kwa wapenzi wa soka ila kwanini iwe 32..si bora ingekuwa mabingwa wote wa mataifa yao wacheze
Nakuona wewe ndiye mfalme giza unajiendea tu na kubet kwako🤣
 
Kwa hiyo UEFA champions league haitakuwepo Tena au [emoji848][emoji3][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Africa timu 5.. Napiga hesabu watachukuliwaje.. Mshindi wa champions league na confederation..
Bado wa3
Finalist wa Champions na finalist wa Caf alafu mmoja ni bingwa wa third runners wa izo tournament mbili 🤔
 
Kwa hiyo UEFA champions league haitakuwepo Tena au [emoji848][emoji3][emoji91][emoji91][emoji91]
Nahisi wanafanya maboresho kutoka kwenye mashindano ya awali, ambayo yalikuwa yanawahusisha vilabu ambavyo ni mabingwa wa mabara yao. Hivyo nahisi hata namna ya kupata wawakilishi inaweza ikabadilika kimfumo toka kwenye huu wa awali (champions league)

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom