Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,455
- 5,134
Watu tofauti wamelalamikia video za mapokezi ya timu ya taifa ya Senegal walipofika kwenye kiwanja cha ndege nchini Marekani, inasemekana walipekuliwa na kuhojiwa kupita kiasi, nahodha wa timu yao alihojiwa kwa saa 3 kabla timu kuruhusiwa kuingia nchini humo.
Ikiwa zimesalia Siku 2 kabla ya kuanza kwa kombe la Dunia litakalofanyika kuanzia Juni 11, 2026 nchini Marekani kuibuka vimbwanga vya aina yake ikiwemo na Mwamuzi kuzuiliwa kuingia Marekani huku kukiwa na tukio hili la Timu ya Senegal kukaguliwa na Nahodha wa Timu kuhojiwa hali inayozua maswali mengi juu ya mazingira na uhuru wa kuchezwa kwa Michezo hiyo
Pia soma: Mwamuzi wa Somalia, Omar Artan, azuiwa kuingia Marekani, kuchezesha Kombe la Dunia 2026