Kombe la NBC Premier League laibukia Nigeria

bakundande jr

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2021
Posts
507
Reaction score
672
Ikiwa ni siku chache baada ya kombe jipya la ligi kuu soka Tanzania bara maarufu kama NBC PL kutambulishwa rasmii na hatimae kukabidhiwa kwa bingwa wa mashindano hayo kwa msimu wa 2022/23 ulitamatika siku chache zilizopita.

Maajabu yametokea hii leo wakati wa utambulishwaji wa kombe jipya la ligi kuu nchini Nigeria ambapo mchezaji wa Zamani Katika ligi kuu ya Nchini Nigeria (NPFL) Victor Ezeji alipewa fursa ya kutambulisha wakati wa kukabidhi kombe kwa bingwa wa ligi hiyo ambae ni Enyiba. Kombe Jipya la Ligi hiyo ni kuwa kombe hilo linafanana na lile lililotambulishwa siku chache zilizopita nchini Tanzania.

Tukio hilo limesababisha kuibuka kwa maswali baina ya wanamichezo. Inakuwaje kombe aina moja litambulishwe katika mashindano tofauti ndani ya siku chache? Ni nani amemuiga mwenzake ama ni makombe ya hisani.

Ni yapi maoni yako maoni kama mdau wa michezo ukizingatia kuwa kombe ni moja ya utambulisho wa mashindano husika.

NB: Ikiwa tuliweza kubadilisha lugha tukapata wimbo wa taifa sidhani kama inashindikana kutoa copy ya kombe la jirani

Hv tulishindwa kuchukua vile vyetu vyetu tukabuni kombe mfano nembo ya taifa,mount kilimanjaro, wanyama etc. Au chochote kinachotutambulisha kama tanzania.
 
Hv tulishindwa kuchukua vile vyetu vyetu tukabuni kombe mfano nembo ya taifa,mount kilimanjaro, wanyama etc. Au chochote kinachotutambulisha kama tanzania.
Kwa kile kinachoonekana ni kiashiria cha kukosa ubunifu kwa wenye mamlaka. Kwa kukopi huku ligi hairakuwa na utofauti na ndondo in term of identity
 
Hv tulishindwa kuchukua vile vyetu vyetu tukabuni kombe mfano nembo ya taifa,mount kilimanjaro, wanyama etc. Au chochote kinachotutambulisha kama tanzania.
hapo kwenye wanyama waweke Mbwa wa COASTAL na sio Lioness
 
Hv tulishindwa kuchukua vile vyetu vyetu tukabuni kombe mfano nembo ya taifa,mount kilimanjaro, wanyama etc. Au chochote kinachotutambulisha kama tanzania.
Wangebuni lenye rangi na mfanano na TANZANITE ndio fahari yetu.
 
wanayanunua ukienda China yapo mengi.

ni mabati tu kama ya kuezekea nyumba ila yanakua na geuge nene wanayakunja linakua kombe la NBC,mwaka huu mbona watu wamepatikana,Loh,,!😅😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…