bakundande jr
JF-Expert Member
- Oct 22, 2021
- 507
- 672
Ikiwa ni siku chache baada ya kombe jipya la ligi kuu soka Tanzania bara maarufu kama NBC PL kutambulishwa rasmii na hatimae kukabidhiwa kwa bingwa wa mashindano hayo kwa msimu wa 2022/23 ulitamatika siku chache zilizopita.
Maajabu yametokea hii leo wakati wa utambulishwaji wa kombe jipya la ligi kuu nchini Nigeria ambapo mchezaji wa Zamani Katika ligi kuu ya Nchini Nigeria (NPFL) Victor Ezeji alipewa fursa ya kutambulisha wakati wa kukabidhi kombe kwa bingwa wa ligi hiyo ambae ni Enyiba. Kombe Jipya la Ligi hiyo ni kuwa kombe hilo linafanana na lile lililotambulishwa siku chache zilizopita nchini Tanzania.
Tukio hilo limesababisha kuibuka kwa maswali baina ya wanamichezo. Inakuwaje kombe aina moja litambulishwe katika mashindano tofauti ndani ya siku chache? Ni nani amemuiga mwenzake ama ni makombe ya hisani.
Ni yapi maoni yako maoni kama mdau wa michezo ukizingatia kuwa kombe ni moja ya utambulisho wa mashindano husika.
NB: Ikiwa tuliweza kubadilisha lugha tukapata wimbo wa taifa sidhani kama inashindikana kutoa copy ya kombe la jirani