Orketeemi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 5,063
- 12,866
Matokeo : BDF XI 2 - Yanga SC 1
============ Yanga imesonga mbele kwa jumla ya magoli 3-2
============
Mechi za kombe la shirikisho barani Afrika kwa ngazi ya vilabu zinaendelea mwishoni mwa wiki hii.![]()
Wawakilishi wa Tanzania Bara Young Africans SC watakuwa ugenini nchini Botswana wakimenyana na BDF XI ya nchini humo ikiwa ni mechi ya marudio hatua ya awali.
Mechi hii ya leo itachezwa ndani ya uwanja wa Lobatse uliopo mji wa Lobatse, kutoka Lobatse hadi Gaborone mji mkuu wa Botswana ni takribani kilometa 75.
Ikumbukwe Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo tayari ikiwa kibindoni na magoli mawili iliyoyapata katika mchezo wa awali uliochezwa Dar es Salaam, huku pia ikiwa na ushindi wa mechi mbili mfululizo katika ligi kuu bara.
Hali ya hewa ya mji wa Lobatse kwa siku ya leo ni jotoridi la wastani wa nyuzi 21 huku kukiwa na jua kiasi, vipindi vifupi vya mawingu huku upepo ukivuma kwa kasi ya 13km kwa saa.
Mechi itaanza kuchezwa saa 2 usiku kwa masaa ya Tanzania.
BDF XI - Yanga SC
(Agg: BDF XI 0 - 2 Yanga SC)
MUDA
2000HRS EAT
![]()
NOTE: Mechi hii itarushwa moja kwa moja na kituo cha Azam Two
(Livestream:http://196.41.40.253/flash.html)
Mungu Ibariki Yanga, Mungu Ibariki Tanzania
Matokeo ya Mwisho: BDF XI 2 - 1 Yanga Afrika (Aggregate 2-3)
**Yanga imefuzu kwa hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho