Kombe la Shirikisho: Medeama yaifunga Yanga 3-1 hatua ya makundi

Kombe la Shirikisho: Medeama yaifunga Yanga 3-1 hatua ya makundi

Bora hata wangeenda kauzu fc, yaani yanga walikuwa wanatafuta mpira kwa torch, hadi huruma
 
umenikumbusha na kile kibwagizo cha miaka ya 90 tulikua tukiimba:
yanga kainaama, medeama kam ..... dole
Hahaha huo ulikuwa ni Noma... Fujo lazima... Kuna Mmoja Tulikuwa Tunamuimba kipa peke yake tu..

''Golikipa'' wengine wanaitikia ''Mzee'' Huku Mnapiga Makofi kila baada ya sekunde Mbili
''kainama'' mnaitikia ''Mzee''
''kainuka'' Mnaitikia ''Mzee''
Wote tunamalizia ANAONA HAYA HUYO...hapo kama yupo karibu mnampiga Masinki na kama Mnamjua kwa Jina lake pale kwenye kiitikio cha Mzee hamsemi Mzee mnaweka jina lake
 
1469560972164.jpg
 
Yanga imejaa Wachezaji, Makocha, Wakufunzi wenye mbinu na weledi wa KUFUNGWA mechi za kimataifa. Siku ikiamriwa Bingwa ni yule aliefungwa mechi nyingi zaidi za kimataifa Yanga itazoa vikombe vingi sana.
 
Kinachonichoshaga na hizi timu za bongo (Simba, Yanga, Azam na Taifa Stars in general) ni jinsi wanavyokuwaga wanapewa HYPE kwenye vyombo vya habari wakati uwezo wao hata hauvutii kuuangalia kwenye TV. Ninachek mechi ya Yanga hapa mpaka ninawaonea huruma. Wachezaji ninaowasikiaga wanasifiwa hata sioni uwezo wao, muda wote wanaangukaanguka tu (hata ukiangalia maumbo ya wachezaji wa nchi za wenzetu ni makubwa tofauti na wachezaji wetu achilia mbali uwezo). TFF lazima ijiangalie upya wapi wamekosea ili warekebishe. Tunacheza mpira wa hovyo sana na wachezaji hawana afya kabisa, sijui wanafanyaga mazoezi/wanalishwa vitu gani. TZ tumejaliwa mashabiki tu na sio wachezaji (Timu).

Unapoizungumzia simba usiichanganye na vitu vya ajabu kama yanga.
 
Wanasimba wenzangu tuwe makini ukijichanganya unakula ban, ndani ya uzi kama huu siku ya TP Mazembe na jamaa ulinigharimu.

Hata hivyo, hawa ni vibonde wa kimataifa, kitendo cha kufungwa na timu ndogo inayoshika nafasi ya 10 kwenye msimamo ni fedheha kwa Taifa. Bingwa kaenda kupigwa 3 na kibonde wa kutupwa.

"Kweli hainaga ushemeji tunakulaga, zamu yako itafika baharia wangu usijali. Coastal Union kapita, Mo Bejeila kapita, Mazembe naye kapita. Tunakulaga, hainaga ushemeji tunakulaga, Medeama naye kapita [emoji1] [emoji2] [emoji2]" by Man Fongo.
 
Ni aibu mkuu, almost muda wote wanaoanguka ni wachezaji wa Yanga tu. Timu pinzani ni nadra sana kuona wamezidiwa nguvu (kuanguka au kuumia). Na hali hii sio kwa Yanga pekee bali ni timu zote za TZ including Taifa Stars. Sijui tumekosea wapi. I think ni mazoezi na diet hafifu pamoja na kulewa sifa.
WALISTUKIA GOLI NYINGI wakawa wanapoteza muda kiaina
 
Back
Top Bottom