Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Ukiwa Mwanasimba uko mitaani ukatamka neno utopolo basi unacheka, unafurahi , unadharau na kubeza , simba ikija uwanjani inaanza mbwembwe Debora anazungusha watu dimba la katikati watu wanakaanga chips shwaaa, raha iliyoje, mara Zimbwe Jr anageuka kwa madoido watu weweee, Kibu anaruka ruka na kunyanyua mikono juu kuamsha shangwe za mbumbumbu, makolo oya oya wanapiga kelele kubwa, Kijili anapiga jaramba na kupokewa kwa vifijo na nderemo za makolo, hapo utopolo kimyaaaa, wanawinda tu huku wakiisaka shingo, mara ghafla bila taarifa kisu kikali aina ya utopolo kinarukia shingo ya Simba , kinachinja, kinachuna ngozi na kukatakata utumbo na firigisi Simba huyo chali, anakoroma na kupiga mateke ya mwisho na kukata roho, kwisha habari yake.
Dawa ya Derby ni moja tu, Simba kukubali imezidiwa uwezo, maarifa na ufundi na Yanga na sasa ijitafute upya otherwise sisi utopolo tutatafuta derby na Gor Mahia ya Kenya au Real Madrid ya Hispania maana hapa bongo hatuna mpinzani, kuifunga Simba mara nne si kubahatisha tena dhahiri ni uwezo mkubwa wa wachezaji wetu.
Kabla ya kumlaumu kipa "Camera", Chief Mangungo au Semaji la dunia au yule kocha mbongo asiebadilishwa Matolu , hebu tujiulize pale kolokoloni kuna mchezaji gani mwenye kiwango kama Max Nzengeli au Baka au Boka?
Simba ijipange tena maana marudiano tutachinja hadi watoto wa Simba na Mama Simba maana safari hii tumemchinja baba Simba!!
Kila mwanayanga alijua Yanga hii yenye ubora mkubwa itashinda derby japo hatukujua magoli yatakuwa mangapi, huku makolo mbumbumbu wakijidanganya wataiweza Yanga hii yenye ubora mkubwa sana.
Simba anzeni tena kujenga upya timu yenu, nunueni wachezaji wengine wazuri, tafuteni kocha mwingine mwenye kiwango, fumueni uongozi, kutafuta mchawi na visingizio hakutaisaida kuifunga Yanga hii ya Master Gamondi!!
Timu bora ya Yanga imeshinda timu mbovu ya Simba, mengine yote ni taarabu tu!!
Kama kawaida niko maskani Buza Mpalanger nawazoom tu Makolo wakilia lia na kusema "baba aomba pipi!" Baba Yanga anajibu hebu kunywa "mma" ukalale!!