Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
TIBA MBADALA NA BUJIBUJI
Hamna kitu inakera kama kwenda ugenini huku ukijua wazi kabisa kuwa miguu yako inatema chechex hadi moto unaweza kuwaka kwa harufu Kali.
Kama unajijua unapitia tatizo hilo hamna noma, Bujibuji's Remedies inafanya kazi kwa ajili yako.
Chukua buku mbili yako, ingia kwenye kiduka cha Mangi, agiza pombe yoyote kali, hizi za buku mbili mbili. Ukiweza chukua na pair moja ya soksi mpya.
Vua ndula zako osha miguu kisha iache ikauke. Tumia leso au pamba kupaka hiyo pombe miguu yako . Paka na paka tena hadi miguu ikate kabisa harufu. Vaa soksi yako mpya kisha nenda ukweni utakuja nishukuru baadaye.
Pombe kali huua bacteria na kuondoa unyevu uliopitiliza. Pia waweza kumimina pombe kali kwenye chupa ya spray na ukawa unaipulizia miguu yako mara kwa mara na harufu itakukimbia.
Pia waweza kuimimina pombe kali kwenye beseni kisha ukadumbukiza miguu yako na kuiloweka humo kwa dakika 1O hadi 15. Toa miguu majini, ianike sehemu yenye hewa ya kutosha na kavu, iache miguu ikauke. Ikikauka vaa soksi zako kavu na safi, kisha nenda popote ukafurahie maisha.