presider
JF-Expert Member
- Feb 26, 2013
- 1,320
- 1,738
Unamfahamu Mzee Lawi Nangwanda Sijaona? Leo angekuwa anatimiza miaka 90. Tupate wasifu wake ulioandikwa na Kamaradi Victor Richard
_______
KOMREDI LAWI NANGWANDA SIJAONA: MZALENDO, MWADILIFU NA MTUMISHI MCHAPAKAZI ALIYESAHAULIWA
Januari 28 kila mwaka hutimia mwaka mpya tokea Taifa letu likumbwe na Msiba Mzito wa kumpoteza Shujaa wetu, Mzalendo wa Kupigiwa Mfano, Mwananchi Mwadilifu na mwenye kujali Utu, Kindakindaki wa Tanzania aliyeipenda Nchi yake kwa dhati, Mchapakazi na Mtumishi asiyechoka, Komredi Lawi Nangwanda Sijaona aliyetutoka Duniani Tarehe 28, Januari Mwaka 2005.
Sitashangaa kama Msomaji wa Maandishi haya hutaweza kumtambua Mtumishi huyu wa Kutukuka kwa kuwa Miundo na Mifumo ya Elimu ya Taifa hili haiwezeshi Watu wema na waliolitumikia Taifa hili kwa Uzalendo wa hali ya Juu kama Komredi Lawi kukumbukwa, kuenziwa na mema yao kurithishwa kizazi hadi Kizazi.
Lawi Nang'wanda Sijaona ni mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika, akifanya kazi kubwa ya kuasisi vyama vya siasa vya ukombozi, tangu TAA, TANU na hatimaye CCM. Alikuwa kiongozi na mzalendo wa mfano wa aina yake, Akifanya mambo mengi makubwa na ya kukumbukwa hapa nchini.
Hakuwa "Fisadi", "Mwizi" wala "Mla Rushwa", alikuwa Mwadilifu na mtu aliyelinda kwa nguvu kubwa Rasilimali za Nchi hii. Kumbe, mwisho wake akafa, akazikwa na mema yote, Akasahaulika!.
Huyu ni Lawi Nangwanda Sijaona, aliyezaliwa Novemba 24, 1928, Chiyanga katika eneo la sasa la Kijiji cha Mnyambe kilichopo Tarafa ya Chilangala, Wilaya ya Newala mkoani Mtwara na kufariki Januari 28, mwaka 2005.
Ni mmoja wa vijana wa Tanganyika waliong’ara katika elimu na kujaliwa kipaji cha uongozi. Akiwa amezaliwa katika familia ya mkulima, Nangwanda alipatia elimu ya msingi Utende kuanzia mwaka 1937 na kumaliza darasa la nne mwaka 1942. Alijiunga na Chuo cha Mtakatifu Joseph Chidya, kilichopo wilayani Masasi mwaka 1943.
Mwaka 1948 alijiunga na Chuo cha Mtakatifu Andrea, Minaki alikopata elimu ya kidato cha tatu hadi cha sita na kuhitimu mwaka 1951. Baadae alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, nchini Uganda kwa masomo ya juu.
HARAKATI ZA UONGOZI.
Nyota ya uongozi ilianza kujichomoza alipokuwa akisoma Minaki. Kutokana na Nidhamu yake na Umaridadi wake, aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Kiranja Mkuu, na pia kusimamia suala la chakula.
Alianza kuandika makala na barua nyingi katika majarida na magazeti mbalimbali kuhusu mambo ya siasa, pamoja na kupigwa marufuku na serikali ya kikoloni.
UANDISHI WA HABARI.
Kutokana na harakati zake, haikuwa ajabu kwa Nangwanda kuanza kazi ya uandishi wa habari mwaka 1952 katika Ofisi ya Sekretari Mkuu, Idara ya Mahusiano kwa Umma na akawa mhariri wa gazeti la kila wiki lililojulikana kama “Habari za Leo”.
Alifanya kazi hiyo kwa miaka miwili hadi mwaka 1954 alipoacha na kisha akaombwa na Halmashauri ya Wilaya ya Newala kuwa mtendaji mkuu wa kwanza katika halmashahuri. Hata hivyo alishika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja tu.
SHUGHULI ZA KISIASA.
Kutokana na mapenzi yake kwa taifa, Nangwanda licha ya kuwa mfanyakazi wa serikali, Novemba 5, 1953, alijiunga na Chama cha Tanganyika African Association (TAA), na kupewa kadi namba 204. Novemba 1955, Rais wa TANU, Mwalimu Julius Nyerere alitembelea Jimbo la Kusini na kufika hadi nyumbani kwa Nangwanda Newala.
Kutokana na kuzuiwa kwake kujiingiza katika siasa, Nangwanda aliweza kufanya shughuli za kisiasa kwa siri kubwa ikiwemo kumkaribisha nyumbani kwake, Mwalimu Nyerere aliyekuwa akianza harakaati za kuikomboa Tanganyika. Mwalimu Nyerere alilala nyumbani kwa Nangwanda pamoja na kushiriki kupanga mipango mbalimbali ya kuikomboa Tanganyika.
Akiwa amedhamiria kuunga mkono kazi ya kupigania uhuru wa Tanganyika, Nangwanda alifanya uamuzi mgumu wa kuacha kazi nzuri serikalini na kujiunga na TANU wakati wote. Mwaka 1955, Nangwanda alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa TANU, Wilaya ya Newala na mwaka mmoja baadae, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TANU Jimbo la Kusini na kuhamia Lindi, yalikokuwa makao makuu ya jimbo.
Nangwanda aliishi Lindi akifanya kazi za TANU wakati wote bila malipo, na wakati huo huo akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU. Katika harakati za TANU, Nangwanda alienda India kikazi, na wakati wa kurejea nchini, ndege ilitua kwenye uwanja wa Nairobi, ambako alishikiliwa kwa saa tatu na askari kanzu wa wakoloni.
MWENYEKITI WA KWANZA MWAFIKA.
Mwaka 1958, Tanganyika ilifanya uchaguzi wa kwanza wa serikali za mitaa, Mpigania uhuru huyu alijitosa kugombea na kuchaguliwa kuwa Diwani na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Lindi. Ushindi huo, ulimfanya kuweka historia ya pekee kwa kuwa mwenyekiti wa kwanza Mwafrika kwenye halmashauri za miji katika Afrika Mashariki.
UCHAGUZI WA KURA TATU.
Nyota ya Nangwanda iliendelea kung’ara na mwaka 1959, wakati wa uchaguzi wa kura tatu, aliteuliwa na TANU kuwakilisha Jimbo la Kusini na akachaguliwa bila kupingwa. Haikushangaza kwamba mwaka 1960, alichaguliwa kuwa Mbunge wa Wilaya ya Lindi.
Mwaka 1965, Nangwanda alirudi nyumbani kwao Newala kugombea ubunge na kushinda kwa kishindo, Ni mbunge wa pekee aliyechaguliwa bila kupingwa katika Wilaya ya Newala katika uchaguzi wa mwaka 1970.
UWAZIRI, UKUU WA MKOA.
Desemba 1961, wakati wa uhuru wa Tanganyika, Nangwanda aliteuliwa kuwa Waziri mdogo wa Serikali za Mitaa na Tawala za Majimbo na baadae alihamishiwa Wizara ya Fedha. Desemba 1962, aliteuliwa kuwa Waziri wa Mila za Taifa na Uongozi wa Vijana.
Aprili 1964, wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais. Utendaji wake bora ulimwezesha kuhamishwa katika wizara mbalimbali zikiwemo za Ardhi, Maji na Makazi. Mambo ya Ndani ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais na Afya na Ustawi wa Jamii.
Mwaka 1972, Wakati wa Madaraka Mikoani, Nangwanda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi na baada ya miezi sita, akahamishiwa Mkoa wa Mwanza. Mwaka 1976 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na mwaka 1980-1983 alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
KUSTAAFU.
Akiwa na umri wa miaka 55, mnamo Machi 1983, aliomba kustaafu. Tofauti na watendaji wengi wa serikali wanaolazimika kubaki mijini, Nangwanda alirudi kijijini kwake Mnyambe, ambako aliishi kama mkulima hadi alipoaga dunia. Hata hivyo, kutokana na uwezo wake wa kuongoza, Machi 1983, alikuwa mbunge wa kuteuliwa hadi Bunge lilipovunjwa mwaka 1985.
MIKUTANO YA KAMATI MBALIMBALI.
Akiwa kwenye harakati za siasa na uongozi wa nchi, Nangwanda alifanya mambo mbalimbali akiwa mwakilishi, ambapo mwaka 1956, aliweza kuwakilisha TANU kwenye mkutano wa Asian Socialist Conference uliofanyika Bombay, India.
Mwaka 1959 alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU na Katibu Mkuu wa kwanza wa Umoja wa Vijana wa TANU.
Pia mwaka huo huo 1959, baada ya kuwa mjumbe wa kuchaguliwa katika Legislative Council (LEGCO) aliteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Kuangalia Muundo wa Serikali ya Tanganyika baada ya kujitawala iliyoongozwa na Sir Richard Ramage, iliyoitwa Tume ya Ramage.
Mwaka 1961, aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano wa Katiba (Constitutional Conference). Mwaka 1961-1962, alikuwa mjumbe wa East African Lagistlative Assembly.
Mwaka 1962, wakati akiwa Waziri mdogo wa Fedha, Nangwanda alikuwa mwakilishi wa Serikali ya Tanganyika katika kamati ya nchi 11 ya Economic Commision for Africa, iliyoteuliwa kushauriana na serikali za Afrika juu ya kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ambayo sasa makao makuu yapo Abidjan, Ivory Coast.
Mwaka 1976, Nangwanda alichaguliwa kuwa mjumbe wa tume ya watu 20 iliyoandaa Katiba ya CCM, na baadaye tume hiyo hiyo iliteuliwa na Rais wa Tanzania, kuandaa Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wa vyama vya hiyari, alikuwa mwanachama wa maisha wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Mwanachama wa Tanzania Tuberculosis and Leprosy Association na Tanzania Wildlife Conservation Society.
Pamoja na kazi kubwa ya kutukuka, inashangaza kwamba historia yake haijulikani kwa Watanzania wengi. Ni wachache mno ikiwemo familia yake inayoweza kuwa na ukweli wote wa maisha ya mwanasiasa huyu.
Hakuna mfumo wa kutunza na kusambaza historia za viongozi aina ya Nangwanda waliolitumikia taifa kwa uadilifu, uaminifu na uchapakazi wa kutukuka
Mola amlaze Pema Mtu Mwema Lawi Nangwanda Sijaona