Katiba ya mafyatu inatoa haki na uhuru kwa kila fyatu kukutana na fyatu yeyote unayemtaka kutembea au kuandamana na unayemtaka, kwenda unakotaka, kusema unalotaka imradi usivunje sheria ya kaya ambayo nayo siyo maagizo au mapenzi ya ndata na wanaowatumia tena vibaya.
Unapozuiwa kufanya hayo hapo juu na mengine kama au kukaribiana nayo, anayefanya hivyo havunji sheria tu bali katiba yetu virakaviraka ya mwaka 47. Kisheria, bila kujali cheo au sura ya yeyote, anayezuia uhuru wa kikatiba ni mhalifu sawa na wahalifu wowote.
Kikatiba, haki na uhuru tajwa hapo juu siyo utashi wala hisani toka kwa yeyote hata awe mnene kiasi gani. Kaya ya mafyatu hutawaliwa kikatiba na siyo kichata wala kichawa. Uhuru ni haki ya kila fyatua.
Msigeuze uhuru kuwa udhuru. Mbona mkipiga njuluku au kuzitumia vibaya hamshikwi na kuswekwa lupango? Mbona mkipiga mnada kaya hamshikani, kufungana, hata kuswekana lupango?