Kondo kutangulia mbele

Peace92

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2013
Posts
261
Reaction score
57
Habari wana jamii forum. Mim Nina ujauzito wa miezi 6 na juz nilipiga utra sound nikaambiwa kondo limetangulia Mbele. Sasa nauliza je kuna madhara gan kondo kutangulia Mbele?au natakiwa nifanye nin?Asanteni
 
AlIsema nirudi mwez wapili kwa uchunguzi zaidi
 
acha ujinga muulize daktari wako ina maana gan na mazara nn? Tatizo watu wengine mnapenda majungu badala ya kumuuliza mtaalamu unaleta majungu utazani madaktari hawaelezi haya mambo. acha majungu
 
acha ujinga muulize daktari wako ina maana gan na mazara nn? Tatizo watu wengine mnapenda majungu badala ya kumuuliza mtaalamu unaleta majungu utazani madaktari hawaelezi haya mambo. acha majungu

Nilimuuliza akasema nirudi mwez wa pili kupima tena! Tafadhal nyamaza tu Kama huna cha kuchangia ndugu
 
Madhara yake ni kwamba unaweza kumwagika damu nyingi wakati wa kujifungua.

Kutokana na kiwango cha lilipo, daktari anaweza kushauri uzae kwa operation.

Kwa hivi sasa unapaswa kuhakikisha kuwa una damu ya kutosha na ukiona dalili yoyote ya uchungu au damu uende hospitali haraka sana. Utakapofika hospitali unaweza kukutana na daktari au mhudumu asiyejua historia yako, utapaswa kumwambia kwa ufasaha na hakikisha unatembea na ripoti toka ka daktari wako.

Nakutakia kujifungua kwema.
 
Wengi hupewa bed rest cjajua kwa nini lakini nahc labda risk ya pre mature labour ni kubwa ukiwa na kondo mbele..so jitahidi upumzike vya kutosha na epuka kazi ngumu....pia ucjali Mungu yupo atakusaidia
 
Pumzika sana usibebe vitu viZito na kama uko kazini ni bora uchukue likizo ukae nyumbani mgegedo pumzika pia kula vitu vyakuongeza dama na ufate masharti ya dr kwabi ukifanya mchezo utampoteza huyo mtt
 
Asanteni sana kwa ushauri ndugu zangu yan mpaka nimeogopa kwa kwel
 
Mimi mwenyewe nimekutwa na tatizo kama lako ila nipo wiki ya 33 na naomba nimegoogle na kuelewa ingawa ntamuona my dr this week na nilivyoelewa ni kama ifuatavyo;
Kondo/placenta kwa kawaida inaweza kuwa positioned nyuma/ posterior au mbele/anterior. Posterior ni normal position na inamaanisha inaanza kondo then mtoto.
Anterior inamaanisha inaanza mtoto then kondo na inasababishwa na factors nyingi, ila sasa it depend kama ni anterior up or lower.

Anterior up haina madhara yoyote na unaweza kujifungua vaginally ila kama utatakiwa kujifungua na kisu dr anatakiwa awe makini cause kumbuka kondo imetangulia anaweza kuikata kondo na kusababisha overbleeding. Na disadvantage nyingine ni utachelewa kumsikia.mtoto akicheza tofauti na mtu mwenye posterior placenta na hata ukimsikia sio strong sana, kumbuka kondo ndo ipo mbele mtoto nyuma.

Anterior lower hii ndo mbaya cause inaziba cervix hvyo there is no way utadeliver normal.lazima kisu/ c-section, kwa kuwa kondo inatangulia kwenye njia chini badala ya mtoto.

NB: all in all hutakiwi kupanick every pregnancy come.on its own way kutangulia au kutokutangulia kwa kondo hakuna madhara yoyote kwa mtoto as long as ultrasound haioneshi any abmormalities kwa mtoto, na siamini kama bedrest ni important kama dr hajakushauri sio muhimu. Hope nimesaidia kwa hilo
 
Asanteni sana kwa ushauri ndugu zangu yan mpaka nimeogopa kwa kwel

Pole dada mi nina mimba miez 6 nina tatizo hilo pia,kondo kutangulia kunasababishwa na vitu vingi baadhi ni kama uliwahi kuzaa kwa operation,na pia abortion,nilishauriwa kutokufanya kazi ngumu,kutosafiri umbali mrefu,kutofanya mapenz,kutoingiza kitu chochote kile ukeni.madhara yake ni kwenye presentation ya mtoto, hatokaa vizuri pia inAweza sababisha mtoto kushindwa kugeuka mwishoni,pia saa ya kusukuma mtoto inaweza tangulia kutoka kondo badala ya mtoto of which is not healthy for the baby ama for u hapo kisu kinakuchungulia,jitahidi kila mwezi kupiga utra sound uone kama linazid kushuka ama linarud normal,mi nimepewa zoezi la kufanya kila siku linalosaidia kondo kurudi kawaida.
 

Kuna gaps kadhaa kwenye hiki ulichoandika.

Uwepo wa placenta anterior or posterior hauna uhusiano na jinsi mtoto alivyokaa. Placenta huitwa anteriror iwapo iko kwenye ukuta wa mbele wa kifuko cha uzazi na posterior iwapo iko kwenye ukuta wa nyuma, hii ni bila kujali jinsi mtoto alivyokaa.

Placenta kuwa posterior haimaanishi kuwa haiwezi kuziba njia ya uzazi. Both anterior and posterior placentae can be praevia.

Both anteriror and posterior placentae are normal. Actually anterior placentae ziko nyingi kuliko zile za posterior.
 
Wengi hupewa bed rest cjajua kwa nini lakini nahc labda risk ya pre mature labour ni kubwa ukiwa na kondo mbele..so jitahidi upumzike vya kutosha na epuka kazi ngumu....pia ucjali Mungu yupo atakusaidia

Pumzika sana usibebe vitu viZito na kama uko kazini ni bora uchukue likizo ukae nyumbani mgegedo pumzika pia kula vitu vyakuongeza dama na ufate masharti ya dr kwabi ukifanya mchezo utampoteza huyo mtt

Ushauri wa kupumzika hauna nafasi kwenye placenta praevia. By the way, neno ""PUMZIKA" ni too general na halitoi ujumbe wowote useful kwa mgonjwa. Vilevile ushauri kama "usibebe vitu vizito" hauna manufaa kwa mgonjwa zaidi ya kumchanganya. Kitu kizito ni nini? Je, wajawazito wasiokuwa na placenta praevia ni sawa wakibeba vitu vizito? je, wanawake ambao sio wajawazito ni sawa wakibeba vitu vizito?

Tujitahidi kutoa ushauri ambao ni tangible and specific!

Ni muhimu mgonjwa akijua kuwa kuna placenta nyingi huwa ziko chini lakini kadri ujauzito unavyokuwa placenta nayo inapanda juu na baadae inakuwa ya kawaida kabisa na mama anaweza kuzaa kwa njia ya kawaida. Kwahiyo cha msingi zaidi ni kufanyiwa check up ili mgonjwa apewe ushauri wa njia na mahali pa kujifungulia, pamoja na viashiria vyote vya hatari.
 
Duuuh Mi nina week ya 31,Ila hata sijui kuhusu position ya kondo....sema nilipitia maumivu flani hapa katikati,nikaambiwa mtoto anageuka... but my next appointment,nitacheck kwa ultrasound......Utakuwa sawa tu,Usijal.
 
Thnks kwa maelezo zaidi as I said mm niligoogle tu bado sijaonana na gyno anipe ufafanuzi.

Ila nina swali nataka kukuuliza kwa experience yako
1) kwa kuhesabu nipo wiki ya 31 na ultrasound za mwanzo zilinisapport, ila nimepiga ultrasound inaniambia nipo wiki ya 33 na 3 days, why is this the case?

2) kwa wiki nilizonazo mtoto anatakiwa awe amegeuza kichwa but ultrasound inasema yupo transverse? Je atageuka au niexpect nn?
 

We haya mambo unayajua kwanza nahisi ndio kazi yako sema ka vile unasikilizia kutoa ujuzi wako...funguka mkuu
 
Ulipewa zoezi gani dada yangu?
 

Ultrasound pekee inayoweza kukwambia umri wa ujauzito ni ile iliyofanywa kati ya wiki ya nane na 13.

Katika kipindi hicho watoto wengi huwa na ukubwa unaofanana. Baada ya hapo kila mtoto anakua kwa speed yake kutokana na alivyorithi kwa wazazi wake pamoja na jinsi anavyopata "chakula".

Katika huyo stage uliyofika kuna uwezekano wa mambo mawili.
1. Inawezekana makadirio yako ya siku za mwisho za hedhi hayakuwa sahihi na hivyo tarehe unazokadiria ziko tofauti na ukubwa halisi wa ujauzito.

2. Inawezekana mtoto anakuwa kwa speed kubwa. Hapa kunaweza kuwa na sababu nyingi, lakini cha msingi zaidi ni kucheck kama hauna ugonjwa wa kisukari ambao ni sababu kubwa ya watoto kuwa na kilo nyingi kuliko ukubwa wa ujauzito.

Kuhusu mtoto kukaa transverse. It is too early kwa sasa hivi kujua final presentation itakuwaje. Watoto huweza kugeuka hata wiki ya 38 na wakakaa kichwa chini. Itakapofika wiki ya 36 ongea na daktari wako kuhusu uwezekano wa kumgeuza mtoto iwapo ataendelea kuwa transverse.

Hatari iliyopo iwapo mtoto ataendelea kuwa transverse ni kwamba chupa ikivunjika kitovu kinaweza kutoka na kusababisha matatizo kwa mtoto. Kwahiyo iwapo chupa itavunjika hakikisha unafika hospitali HARAKA sana.
 

sawa doctor
 
Ngoja nijaribu kukuelezea hilo zoez,ni rahisi,piga magot sakafuni afu inama kama style ya mbuzi kagoma then kifuani weka mto au mito miwili ili kifua kisiwe chini sana then fanya kama unajinyonga nyonga kiuno pande zote,niliambiwa zoezi hili linaweza kuiposition placenta taratibu,unatakiwa ulifanye kila siku angalau kwa 15 min mpk utakapojifungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…