Kondo la Nyuma la uzazi kumtangulia mtoto wakati wa ujauzito

Kondo la Nyuma la uzazi kumtangulia mtoto wakati wa ujauzito

OCC Doctors

Senior Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
113
Reaction score
172
Kondo la uzazi kumtangulia mtoto (Placenta previa) hutokea wakati wa ujauzito, kondo huongezeka ukubwa na kutanuka kadri mfuko wa uzazi unavyotanuka na kukua.

Ni miongoni mwa hali za hatari kwa mama mjamzito ambapo kondo la nyuma hujipachika katika sehemu ya chini ya mfuko wa uzazi, kukua na kisha kufunika sehemu ndogo au kubwa ya njia ya uzazi inayoelekea kwenye mlango wa uzazi na hivyo kuzuwia uwezekano wa mtoto kuzaliwa kwa njia ya kawaida.

Sababu hatarishi zinazo pelekea Kondo la uzazi kumtangulia mtoto (Placenta previa), sababu kuu ni uwepo wa ugonjwa wa shinikizo la damu wakati wa ujauzito, uwepo wa mapacha tumboni, jeraha la moja kwa moja kwenye tumbo, kupasuka mapema kwa utando au chupa la uzazi (PROM), kifuko cha uzazi kuwa na maji mengi (polyhydramnios), na kupasuka kwa utando kunakosababishwa na kupungua kwa ghafla kwa shinikizo la ndani ya mji wa uzazi.

Sababu zingine zinazopelekea kondo kumtangulia mtoto ni uwepo wa uvimbe kwenye kizazi wakati wa ujauzito (Uterine leiomyoma), hasa uvimbe ukiwa uko nyuma ya kondo la uzazi, na sababu ya mwisho ni historia ya awali ya kondo la nyuma kumtangulia mtoto katika mimba iliyopita.

Miongoni mwa dalili ni pamoja na muda wa kugundua tukio hili ni kuaniza wiki ya 32 za ujauzito, ambapo hatua ya kwanza hujitokeza kwa wastani kutokwa na damu ukeni bila maumivu katika miezi mitatu ya kati na miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito. Damu huwa ni nyekundu nyangavu (Bright red blood). Kondo la uzazi kumtangulia mtoto huthibitishwa kwa ultrasound.

380407119_809630264504484_6694643830092347236_n.jpg
 
Back
Top Bottom