secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 2,998
- 4,948
Juzi nilipata taarifa kutoka Kwa mwalimu mwenyeji wa shule ya Kondoa girls kuwa kuwa katika shule yao wizi umekithiri sana, mwalimu yule alidai kuwa watu wasiojulikana wanaenda kuiba mbaazi katika shamba la shule na mbaya zaidi watu wale wameanza kutembelea nyumba za waalimu ili kuiba chchote kitu.
Mwalimu mwenyeji aliniambia kuwa katika harakati za kuhakikisha usalama wa shule wameamua kuwatumia waalimu wa mazoezi (field teachers), nilipomuuliza kuwa Kwa nini wanafanya hivyo alidai kuwa hiyo ni moja kati ya extra curricular activities yaani kufanya hiyo shughuli kunaweza kumuongezea mwalimu alama katika teaching practice hata wakapata GPA nzuri.
Mwalimu aliendelea kusema kuwa endapo waalimu wa field hawatashiriki kikamilifu katika suala zima la ulinzi wanaweza wakapata alama duni kwenye external assessment. Naombeni niwaulize Wana JamiiForums iwapo jambo hili la mwalimu wa field kuamka saa nane za usiku hadi saa kumi alfajiri Kwa kushurutishwani sawa au la ilhali Kuna walinzi wa shule wanaolipwa.
Pia habari za kuaminika zinasema baadhi ya walimu hao wanapiga pasi ndefu yaani wanapata msosi mara moja tu Kwa siku Kwa sababu shule iko mbali kidogo na mjini halafu shule haiwapikii chakula cha usiku 🤣🤣🤣😂.
Karibuni Kwa maoni.