DOKEZO Kondoa Girls High School waalimu wa field wamegeuka walinzi wa shule, usiku kucha hawalali

DOKEZO Kondoa Girls High School waalimu wa field wamegeuka walinzi wa shule, usiku kucha hawalali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Juzi nilipata taarifa kutoka Kwa mwalimu mwenyeji wa shule ya Kondoa girls kuwa kuwa katika shule yao wizi umekithiri sana, mwalimu yule alidai kuwa watu wasiojulikana wanaenda kuiba mbaazi katika shamba la shule na mbaya zaidi watu wale wameanza kutembelea nyumba za waalimu ili kuiba chchote kitu.

Mwalimu mwenyeji aliniambia kuwa katika harakati za kuhakikisha usalama wa shule wameamua kuwatumia waalimu wa mazoezi (field teachers), nilipomuuliza kuwa Kwa nini wanafanya hivyo alidai kuwa hiyo ni moja kati ya extra curricular activities yaani kufanya hiyo shughuli kunaweza kumuongezea mwalimu alama katika teaching practice hata wakapata GPA nzuri.

Mwalimu aliendelea kusema kuwa endapo waalimu wa field hawatashiriki kikamilifu katika suala zima la ulinzi wanaweza wakapata alama duni kwenye external assessment. Naombeni niwaulize Wana JamiiForums iwapo jambo hili la mwalimu wa field kuamka saa nane za usiku hadi saa kumi alfajiri Kwa kushurutishwani sawa au la ilhali Kuna walinzi wa shule wanaolipwa.

Pia habari za kuaminika zinasema baadhi ya walimu hao wanapiga pasi ndefu yaani wanapata msosi mara moja tu Kwa siku Kwa sababu shule iko mbali kidogo na mjini halafu shule haiwapikii chakula cha usiku 🤣🤣🤣😂.

Karibuni Kwa maoni.
Shule kama shule wanashindwa vipi kuajiri mlinzi,kamati ya shule pia wameshindwa kushughulikia swala la mlizi kweli? Ikitokea la kutokea hapo asilaumiwe mtu.
 
Walimu bongo wanadhalilika sana. Yaani ukisoma tu fani ya ualimu hata fundi viatu anakudharau, hata muosha magari anakudharau.

Fani ya ualimu imeshuka sana hadhi bongo. Mara walimu wachangie mwenge kwa lazima, wahudhurie mikutano ya kisiasa kwa lazima, wapigwe viboko hadharani, wawekee lockup na watendaji wa vijiji na mambo ya ajabu ajabu sana. Walimu bongo wanapitia mengi sana.
Sasa hapo wanadhalilika au WANAJIDHALILISHA?! Mosi, Walimu wenyeji ndo wametoa hiyo order kwa Walimu wa Field; yaani Walimu kwa Walimu wanaoneshana masharubu! Pili, hivi msomi mzima unakubali vipi kufanya kazi iliyo nje ya taaluma?! Hapo bado zikitoka ajira, akina dada wengine wanaenda kutoa tunda halmashauri eti ili wasipelekwe vituo vya ndani ndani!
 
Pale kondoa girls Kuna waalimu wawili (makamua na na mwalimu mmoja wa nidhamu mwenye kitamba kama peter Msechu) wanamwendesha sana mkuu wa shule eti Kwa sababu ni mwanamke. Juzi mwalimu yule mweñye kitambi kama Cha Msechu alimkaripia mwalimu mmoja wa kike wa field mbele ya waalimu wengine na wanafunzi kisa hajamwamkia.
 
Kwa hio upoteze mda m8aka miratu halafu upate gpa mbaya. Fursa zingine zinahitaji gpa kubwa mfano kuwa lecture, kupata scholarship nk. Kwa nini upatw gpa mbaya wakati ni mwanafunzi na gpa ni jukumu lako ?.
Ukishapata gpa mbaya hairekebishiki.
Majuto si mjukuu
Nyinyi ndio mnaokubali upumbavu kama huo

Hakuna uhusiano wa GPA na kazi ya kulinda shule

Ni kutojitaambua tu
 
Nyinyi ndio mnaokubali upumbavu kama huo

Hakuna uhusiano wa GPA na kazi ya kulinda shule

Ni kutojitaambua tu
Duh! Madogo wa field wanateseka sana pale, mara wageuke walinzi mara wavune mbaazi, yote hayo ni Kwa sababu tu wanalala kwenye majengo ya shule.
 
JF asante,kazi hiyo nimewahi fanya 1995 ila athari zake kubwa ,niseme nisiseme?
 
Pale kondoa girls Kuna waalimu wawili (makamua na na mwalimu mmoja wa nidhamu mwenye kitamba kama peter Msechu) wanamwendesha sana mkuu wa shule eti Kwa sababu ni mwanamke. Juzi mwalimu yule mweñye kitambi kama Cha Msechu alimkaripia mwalimu mmoja wa kike wa field mbele ya waalimu wengine na wanafunzi kisa hajamwamkia.
Poleni sana. Wewe unavyo-comment inaonyesha wazi ni miongoni mwa hao wanafunzi wa ualimu. Itoshe kusema kwamba waalimu ni kama kondoo. Mna upole wa kishamba. Nadhani tusubiri comment ya Mpwayungu Village labda anaweza kuwa na maoni tofauti.
 
Sijui ni mimi mkorofi au vipi ila kamwe nisingefanya huo undava, acha nipate below to ila noma noma tu.

Uzi usindikizwe na track mbili, Below by Baraka Abayo ft Roma & Chege na Mara Hoo by Bou Nako ft JCB

Dj, plee dat tings
 
Kondoa girls naamini wanaolinda ni walimu wa kiume wa kike hapana Sasa hawapaswi kulaumu kabisa na huu ndio ushauri wangu wa mwisho
Km wanawapa na madenti wawagonge hapo haina shida Ila km ndio pangu pakavu huo ni unyonyaji
 
Back
Top Bottom