Kondomu inayotambua maambukizi ya Zinaa yagunduliwa

Kondomu inayotambua maambukizi ya Zinaa yagunduliwa

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.

Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.

===============================

Kondomu inayotambua maambukizi ya Zinaa
150526121734_condoms_624x351_thinkstock.jpg

Kondomu inayotambua maambukizi ya zinaa

Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.

Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.

150506140327_condoms_ebola_sex_gch_640x360_thinkstock_nocredit.jpg

Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

''tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.
Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .

Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''
''Kwa hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''

150214094907_thai_condoms_640x360_afp_nocredit.jpg

Wavumbuzi hao wanasema kuwa hiyo ni mojawepo ya njia salama ya kubaini usalama penzi lenyu

Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.

Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa "Ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu''

Chanzo: BBC
 
Duh!,kweli duniani kuna mambo!,halafu madogo wenyewe wana umri mdogo.
 
If true, well-done to the team! St. Kayumba wapo bize kuhudhulia mikutano yaKinana! Mwishowe wanabakia kuingia siasa na namba waliikimbia, wanabakia kupigamakofi na kuitikia ndiyooo kwa vile walisha zoea kulishwa sumu tangu utotoni,maarifa hamnazo mtaweza vipi namba? Sayansi mtaishia kiuisikia tu!
CCM Oyeee!
UFISADI Oyeee!Kulindana Oyeee!
Chama kwanza, wengine baadaye!
 
Huku kwetu hata maprofesa wa fani za sayansi wanakimbilia siasa, na wanajifunza kuremba maneno!
 
Watu tumechoka kutumia mifuko, watafute dawa waache ubishoo.
Unaanzaje kwanza kuangalia rangi ya kondom katikati ya mgegendo.?labdo kma unamgonga demu wa kupewa,wa kujitaftia hichi kiti hakiwezekani.
 
Hao hao utawasikia kesho wanasema zina madhara. Wajinga sana.
 
Hongera zao, uzuri wao wazungu ikija upande wa maendeleo they don't care who you are
 
aliyenacho ataongezwaa tu..sie tuendelee kupigana vijembe vya siasa...
 
Mipango ya hela tu hiyo. Mbona hawagundui dawa ya "Ngoma"?
 
Duh!,kweli duniani kuna mambo!,halafu madogo wenyewe wana umri mdogo.

ni wadogo ila hawajagundua,waandishi wamelikuza,wao wame present idea tu na wala idea haijafanyiwa kazi na kutoa product.
 
UDSM wao wamengundua style mpya ya kufanya mapenzi
 
Sasa mmeshaandaana na kunyegezana ina maana utaitumbukiza condom kwanza kuangalia kama ni salama au la?...
Umezama chumvini na kulana mate halafu unaingiza condom kitu kinasoma positive, utalia?...
 
Tusha choka.na madude yao ya kutukinga wa gundue dawa ya ukimwi yatosha mwishowe watakuja kutuvalisha kondomu ya mwili mzima
 
Siku chache zilizopita wanafunzi wanne kutoka shule ya isaac newton academy huko ilford essex uingereza walivumbua na kuunda kondomu yenye uwezo wa kung'amua mtu alieambukizwa maradhi ya zinaa wakati wa kujamiiana kondomu hiyo ya kiume ina uwezo wa kubadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anaeugua maradhi ya zinaa. Kondomu hiyo imepewa jina la S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya chlamydia, kaswende, na kisonono
 
Back
Top Bottom