BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Ikiwa ni hatua ya kuendelea kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema Serikali imesambaza kondomu milioni 111.934 nchini katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2022.
Hayo ameyabainisha juzi Januari 13, 2023 kwenye kikao cha ndani jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa kuhusu kuhuisha na kujumuisha maswala ya Ukimwi mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi.
Dk Mollel alisema kati ya kondomu hizo, milioni 2.8 zimesambazwa kwenye wizara na taasisi mbalimbali.
Amesema Wizara ya Afya imeanzisha huduma ya kujipima maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) mahala pa kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya vipimo vya VVU kwa watumishi mahali pa kazi hasa wanaume.
“Wizara imeanzisha huduma ya kujipima VVU (Jipime) mahala pa kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya vipimo vya VVU kwa watumishi sehemu za kazi hususani wanaume. Hadi kufikia Desemba 2022, watu 86,231 wamepatiwa huduma ya Jipime mahala pa kazi,” amesema.
Mwaka 2020, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alieleza mbele ya waandishi wa habari kwamba Bunge la Tanzania lilirasimisha sheria ya wananchi kuweza kujipima wenyewe maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).
“Napenda kuwapa habari njema kuwa Bunge la Novemba (2020) limepitisha sheria, kwa hiyo sasa ni rasmi Tanzania mtu kujipima maambukizi ya VVU mwenyewe.
“Kwa hiyo, hivi vitendanishi (vifaa) vitakuwa vinauzwa kwenye maduka, pia kugawa bure baadhi ya maeneo kwa sababu wakati mwingine watu wanaona unyanyapaa kwenda kupima wenyewe,” alisema Ummy.
Hata hivyo, aliweka angalizo kwamba kujipima mwenyewe sio majibu ya mwisho, hivyo amewaelekeza wananchi baada ya kujipima kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya kuthibitisha na ushauri zaidi wa jinsi ya kuishi.
MWANANCHI