Kondomu yavunja ndoa. Huu ni wivu au umakini katika ndoa???

Huyo mwanamke anatakiwa kupimwa akili.... kukuta kondom kwenye suruali ya mumewe ni jambo moja na kutembea nje ya ndoa ni jambo jingine. ni mambo tofauti hayo....LABDA ALIWEKEWA MFUKONI. amtende haki mumewe banaaa..:angry:
 

Hapo reaction yako ikoje ndugu? kama ndio yamakukuta ww. 😛opcorn:
 
Huyo mwanamke anatakiwa kupimwa akili.... kukuta kondom kwenye suruali ya mumewe ni jambo moja na kutembea nje ya ndoa ni jambo jingine. ni mambo tofauti hayo....LABDA ALIWEKEWA MFUKONI. amtende haki mumewe banaaa..:angry:

Sasa nimepigiwa simu kuwa mwanamke kaenda kumtafuta Daktari aliyedaiwa kutoa kondomu hizo. Sijui mambo yatakuwaje huko, na sijui reactipon ya mwanaume juu ya hilo!!! Nitawajuza nikizipata news!!!
 
Hapo reaction yako ikoje ndugu? kama ndio yamakukuta ww. 😛opcorn:

Mi napenda mtu awe mkweli,in case yamenikuta tuzungumze tu kwanza,manake kuna sababu ya yeye kwenda nje....lakini anapoleta uongo juu ya uongo eti anazuia mimba,akaenda kwa Dr akakuta zimebaki mbili....hapo hatutaelewana kabisa,hapo inaonekana hayuko tayari kukabiliana na tatizo lililopelekea kwenda nje bali yeye anaendelea na uongo wake,kwa minajili hiyo namruhusu aendelee ila atimize majukumu yake mengine,mi naye basi........:coffee:
 
Kama siyo wivu kwanini usiamini kuwa kweli kazitoa hospitali hizo kondomu????

Kama ishu ni kuzuia uzazi na mhusika ni mimi pia,tungekuwa tumeshirikishana na kuamua namna ya kupanga uzazi,nami hapo wala singeshtuka.........read between the lines ya excuse ya huyo mwanaume utanielewa.
 
kwani kondomu zenyewe zilikua aina gani raha,raffrider,dume, salama au mcd?
 
Je wewe unadhani utamkuta mwanaume aliye straight atakaye kuambia kwamba anakwenda ku-do! subiri :clap2:

Sidhani na sitoweza subiri kujua kwakuwa mimi ni MTAWA.:clap2::coffee:




 
Kukutwa na condom mbili ni kosa,zingekuwa 3 wife angemuelewa,sasa alitegemea kutumia hizo mbili kwa siku ngapi si za siku moja tu ? Kuna jamaa alikutwa na condom mfukoni na alipoulizwa akadai kuna shindano Clouds radio watangazaji wanazunguka mitaani na anaekutwa na condom mfukoni anapewa laki 1 ndio maana anazo wife akakubali na kuomba akipata hiyo laki amgawie nusu hahaha! kuna watu wabunifu kweli hapa bongo.
 

huyo mwanamke ana mikogo, mumewe anamlinda yeye analeta jeuri, si wanasema eti " ukimpenda utamlinda".

 
hicho kisa kimenikumbusha zamani kidogo mimi nilienda kwa boyfriend wangu mkoani kwa siku kadhaa, siku mbili kabla ya kuondoka nikiwa nachukua nguo zangu chafu kwenye kapu nifue,enheee chini kabisa nikazikuta ndomu boksi zima la msd,mimi na yeye tulikuwa hatutumii kwa kuwa tulikuwa na utaratibu wa kupima mara 3 kila mwaka as tulikuwa tunaishi mbalimbali, nilipomuuliza akadai ofini kwao walitembelewa na waelimishaji wa ukimwi na kila mtu akapewa boksi zima!???mwisho siku nikamwambia mungu asante ni;ivyoondoka ndio ukawa mwisho wa habari....
 

:clap2::clap2::clap2::clap2::coffee:
 
michelle usinicheke mwenzio!!yalinikuta nikashindwa hata kulia zaidi ya kujuta kilichonitoa kwetu hadi huko maporini then dahhhh

Nailyne wangu sijakucheka,tunapita kwingi,nimekupa makofi kwa kuchukua hatua nzuri.....yaani umenifurahisha sana....

Napenda watu wanaoona jambo then wanachukua uamuzi mapema kabla hayajawakuta makubwa zaidi.:coffee:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…