Kumekuwa na malalamiko ya watu kadhaa kwamba Kondomu za Kampuni ya Bull Zinapasuka sana. Baadhi ya wadau wanaona Kondomu hizo si salama ni laini sana kiasi kwamba hupasuka kirahisi wakati wa tendo la kujamiiana.
Ukweli upoje?
Ukweli upoje?
- Tunachokijua
- Agosti 9, 2022, mdau wa JamiiForums alianzisha uzi wenye kichwa cha habari “Kondomu za BULL zinapasuka, ni hatari” ukifafanua kupungua kwa ubora wa kondomu za Bull.
Baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wadau kadhaa kuhusu kupasuka kwa Kondomu za Bull Jamiiforums ilifanya mazungumzo na TMDA ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo.
TMDA ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara Udhibiti wa Vifaa Tiba ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi nchini imegusia kuhusu madai hayo.
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa TMDA, Gaudensia Simwanza anaelezea uhusu madai hayo:
“Bull Condoms ni moja ya biadhaa ambazo tunazifuatilia sokoni, hatujapata kesi ya aina hiyo na tafiti zetu zinaonesha kuwa zina ubora mzuri
Inawezekana mtumiaji au watumiaji waliolalamika hakuzingatia katika kuhifadhi na matumizi sahihi, ukifanya tofauti ni rahisi kupasuka.
Unajua kuna ukaguzi na ufuatiliaji, vyote tunafanya, lakini hatukatai kupokea malalamiko, na ikibidi watusaidie kujua ‘batch’ namba ngapi au ni maeneo gani ndiyo tunaweza kufuatilia.”
Aidha, amebainisha kuwa ni ngumu kuhukumu Bull Condoms zote kwa tatizo moja au la watu wachache ambao pia hawajaweka wazi ni wapi na lini.
Amesema kuwa taasisi hii husisitiza kuhusu matumizi sahihi na pia kondom hazitakiwi kuwekwa kwenye jua au katika mazingira ambayo si rafiki.
Nini cha kufanya ikiwa kondomu itapasuka?
Kuna baadhi ya mambo ya msingi unayoweza kufanya ikiwa kondomu itapasuka kwa bahati mbaya wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa BBC, mambo haya manne ni muhimu kuyazingatia:
- Kuwa mtulivu na baadae tafuta kondomu hiyo iliopasuka. Mara nyengine vipande vya mpira huo wa kondomu unaweza kuingia ndani ya mwili.
- Tumia dawa za kuzuia kushika mimba iwapo hamjakubaliana kupata mtoto pamoja. Dawa hizi zinapaswa kutumiwa katika kipindi cha saa 72. Zinauzwa dukani-ikimaanisha kwamba zinapatikana katika maduka ya dawa.
- Kupimwa magonjwa ya zinaa hususan VVU iwapo hujui hali ya mwenzako. Nenda katika kituo cha dharura karibu nawe na umwambie daktari yaliofanyika. Unaweza kutumia dawa za dharura za kuzuia maambukizi ya VVU.
- Chunguza kilichotokea. Wapenzi wengi huruka hatua hii. Hayo ni makosa makubwa, kwa sababu ni hadi utakapoelewa ni kwa nini mpira huo ulipasuka ndiposa unaweza kujiweka katika hatari nyengine. Hivyobasi jiulize swali hilo.