Kondoo 17 wauawa, watano wajeruhiwa na fisi wanne Itilima

Kondoo 17 wauawa, watano wajeruhiwa na fisi wanne Itilima

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
Hofu imetanda kwa wakazi wa Kijiji cha Gambasingu wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu baada ya fisi wanne kuvamia zizi la kondoo na kuua mifugo 17 huku wengine watano wakijeruhiwa katika shambulio la usiku wa manane, leo Agosti 20, 2025.

Shambulio hilo lilitokea majira ya saa sita usiku katika Kitongoji cha Mwabasambo A na limeelezwa na wenyeji kuwa ni tukio la kihistoria kutokana na idadi kubwa ya mifugo kushambuliwa kwa wakati mmoja.

Singisi Mgina, mfugaji aliyeathirika, alisema fisi hao walivamia zizi lake kwa kasi na kuua kondoo kabla hajapata msaada.​

“Walivamia ghafla na kuua kondoo kwa muda mfupi. Nilipopiga kelele wananchi walifika lakini tulishindwa kuwafukuza. Hasara yangu ni kubwa, inafikia Sh milioni mbili. Kondoo hawa ndio chanzo cha kipato cha familia yangu,” alisema kwa masikitiko.​

 

Attachments

  • IMG-20250820-WA0131.jpg
    IMG-20250820-WA0131.jpg
    804.8 KB · Views: 45
  • IMG-20250820-WA0132.jpg
    IMG-20250820-WA0132.jpg
    202.6 KB · Views: 54
  • IMG-20250820-WA0133.jpg
    IMG-20250820-WA0133.jpg
    150.2 KB · Views: 47
Bora wale hao kondoo, waache kula watoto wadogo.
 
Back
Top Bottom