- Source #1
- View Source #1
Kuna huu uzi nimukutana nao umenikumbusha nilikua mdogo nilikua naambiwa sana stori za uwezo wa Kondoo kupambana na Radi,
Hapa stephot kwenye uzi wake alisema "kuna kipindi nilipokuwa likizo nilitembelea mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara na Arusha, nilichokigundua ni kuwa wafugaji karibu wote wa Ng'ombe wanakuwa na kundi la Kondoo, nilipouliza niliambiwa kuwa Kondoo wanasaidia kuzuia Radi. Mwenye ufahamu wa kina naomba anifafanulie utaalamu uliopo nyuma ya hii kitu"
Sasa JamiiCheck mtusaidie kuna ukweli hapa?
Hapa stephot kwenye uzi wake alisema "kuna kipindi nilipokuwa likizo nilitembelea mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara na Arusha, nilichokigundua ni kuwa wafugaji karibu wote wa Ng'ombe wanakuwa na kundi la Kondoo, nilipouliza niliambiwa kuwa Kondoo wanasaidia kuzuia Radi. Mwenye ufahamu wa kina naomba anifafanulie utaalamu uliopo nyuma ya hii kitu"
Sasa JamiiCheck mtusaidie kuna ukweli hapa?
- Tunachokijua
- Radi ni mwangaza na miale ya mwanga mithili ya shoti za umeme inayotokea wakati wa ngurumo wa mvua ya radi. Neno radi linaweza kutaja pia sauti yenyewe na mwanga katikati ya mawingu unaweza kuitwa "umeme".
Asili yake ni volteji inayojijenga kati ya mawingu angani yenye chaji tofauti au pia kati ya mawingu na ardhi. Volteji hiyo ikiongezeka mno husababisha mkondo wa umeme hewani unaoonekana kama mwangaza mkali.
Mkondo unatoa pia joto kali na joto hilo husababisha kupanuka kwa hewa ghafla. Upanuzi huo unaleta sauti inayosikika kama ngurumo kama ni mbali, lakini inaweza kusikika pia sawa na mshtuko wa mlipuko kama ni karibu.
Madai
Kumekuwepo na simulizi nyingi kuwa Kondoo ni mnyama mwenye uwezo wa kupambana na kuzuia radi. Je ni uhalisia wa madai haya?
Kondoo hawawezi kupambana na radi na ni rahisi kuathirika nayo. Radi inaweza kuua kondoo papo hapo kwa urahisi, mara nyingi kwa kusababisha moyo au mfumo wa upumuaji kusimama, hasa wanapokuwa katika kundi au wakiwa wamejikinga chini ya mti.
Tovuti ya Epashupalan inabainisha kuwa Wanyama wafugwao kama farasi, punda, kondoo, mbuzi na nguruwe ambao hufugwa kwa urahisi kwenye malisho ya wazi au nyanda za majani, huwa na tabia ya kukusanyika chini ya miti wakati wa dhoruba na hivyo wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kupigwa na radi.
Madhara hatari ya radi ni pamoja na kuungua, kuharibika kwa ngozi na manyoya, nyama, mifupa, tumbo kujaa gesi, kusimama kwa moyo, uharibifu wa mishipa ya fahamu, na mengineyo.
Mfano Machi 01, 2016 tovuti ya Mwananchi iliripoti tukio la Kondoo 12, Ng’ombe 20, na mbuzi wawili mali ya Okola Magige kutoka mkoani Mara walikufa kwa kupigwa na radi katika Kijiji cha Burunga wilayani Serengeti.
Kadhalika mwaka 2020 tovuti ya NepalTimes iliripoti idadi kubwa ya kondoo waliokuwa wakichungwa katika malisho ya juu milimani waliouawa kwa radi kali katika wilaya ya Jumla nchini Nepal.
Vilevile Chama cha Hali ya Hewa cha Marekani kinaeleza tukio la kihistoria ambapo, Julai 22, 1918 Radi iliua kondoo 504 katika Msitu wa Kitaifa wa Wasatch huko Utah.