Baraka Kasinge
Member
- Apr 4, 2016
- 60
- 69
Kondoo wawili walikuwa wakitokea pande tofauti za mto. Mmoja akitokea kusini na mwingine kaskazini, na kila mmoja alihitaji kuvuka ili kuelekea upande wa pili.
Walipoufikia ule mto, kwa bahati mbaya, mto ule haukuwa na daraja pana, zaidi ya gogo lililokuwa limelazwa kwa kuvukia.
Cha kushangaza, 😳kondoo wale walipolifikia (lile gogo) wote walilazimisha kuvuka kwa pamoja.😳 Baina yao, hakuna hata mmoja aliyekuwa tayari kusimama ili mwenzake apite kwanza.🫢
Hatimaye walikutana katikati ya lile gogo, na bado, walilazimisha kupishana. Kwa bahati nzuri, kama si mbaya,🤣 gogo like halikuwa na nafasi ya kutosha wao kupishana. Hivyo, wote walijikuta wameteleza na kisha kuangukia mtoni wakasombwa na maji.🤦🏽♂️
Funzo: Tunaposhindana kukomoana, tusisahau kujiuliza kitakachotukumba ikiwa tutashindwa. Hata kama tutashinda, bado tusisahau, kukomoana huzaa uhasama, na visasi. Mwishowe, mashindano, huzua msiba.😭
Upvote
1