Marigwe
Member
Join Date: Fri Nov 2009
Posts: 18
Thanks: 0
Thanked 14 Times in 8 Posts
Kabla ya kongamano hilo kukutana, nilikuwa nimejaa na matumaini kwa kijana Nape Nnauye nikawa nimeamua kama mkazi wa Ubungo, kumpigia kura ya maoni kwa ajili ya jimbo la Ukonga.
Marigwe hajatuambia kwa nini alikuwa na matumaini na Nnauye.
Lakini baada ya kongamano lile nimeghairi. Nimetambua Nnape is just a philosopher/theoretician academician kama Baregu na Dr Azaveri Lwaitama. They are good at criticising only kama mashabiki wa mpira wa Kitanzania ambao wanajiona wao ni bora zaidi ya Maximo.
Anachanganya ku-criticize na kujiona bora. Sio lazima critic awe bora ya yule anayekuwa criticized. Sote tunaweza kuwa katika quagmire ya kutojua jibu la hesabu, lakini hili halimaanishi kwamba wewe ukitoa jibu lisilo kweli nitashindwa kujua.
Kwa mfano, naweza nisijue jibu la hesabu ya kujumlisha, lakini nikajua kwamba namba zinazojumlishwa zote ni even, na ukijumlisha namba even utapata jibu even, kwa hiyo hata kabla sijajua jibu lenyewe, ukiniletea jibu lililo odd, nitajua kwamba jibu si sahihi.
Critics wa Kikwete hata kama hawana uwezo wa kuongoza nchi wanaweza kujua jinsi gani hatutakiwi kuendesha nchi. Let us not try to silence a much needed force of dissent.
Ukimpa Nnape aongoze hataweza. Mimi nayasema haya from experience.
OK, hebu tusikilize experience gani hii?
Tunaemjua Jackson Makwetta enzi zake kabla hajawa Mbunge akifundisha IDM naye alikuwa hivi hivi kama akina Baregu na huyu kijana Nnape. Leo Makwetta ana miaka 30 ndani ya jimbo Njombe kaskazini wapiga kura hata kumuona hawataki. Hilo la kwanza.
Sasa experience yako na Makwetta unaenda kumvika Nnauye wapi na wapi? Isn't this a case of a dilapidated comparison?
La pili nielezee kongamano. Hilo kongamano mwanzoni nilifikiri limeitwa kwa ajili ya kuzungumzia mustakabali wa taifa within the context of the changing times and trends ndani ya utandawazi. Ah wapi Bwana kumbe ilikuwa ni mkusanyiko wa wazee ambao walikutana na kulia, kulalamika na kumlaumu kijana JK.
Kama wazee wanaongelea performance ya rais, how can that not be about mustakabali wa taifa? Au mnataka mpaka awe Nyerere anawatungia watu vitabu na kuwasema ndiyo muone statesmanship, akifanya mwingine bila muhuri wa Nyerere ni nostalgic jealousy?
Na wakaamua kumchapa Lowasa lakini hawakuwa na ujasiri wa kumtaja hata kwa jina.
Hujaeleza umejuaje ni Lowassa wakati hakutajwa jina, unatupa shaka na uwezo wako wa kujieleza.
Basi wangemwalika ahudhurie. Sisi tunaoijua historia ya nchi yetu tunafahamu kuwa hao wazee ndiyo walioweka msingi mbovu wa utawala kiasi kwamba leo akina JK wanahangaika.
Kwamba wazee wameweka misingi mibovu kwa wajuvi halina mjadala kama mvuto wa dunia, lakini JK anahangaikaje? JK amekuwa madarakani takriban miaka minne sasa, amefanya nini kubadilisha misingi mibovu hii?
Mimi ambaye Baba yangu alifanya kazi enzi za Nyerere wakati akina Butiku wakiwa ndiyo Private Secretary wa Rais, tunakumbuka alivyojenga himaya enzi zile. Butiku alikuwa very powerful kuliko hata Katibu Mkuu Kiongozi. Sasa akikumbukia enzi hizo lazima atakuwa nostalgic. Enzi zile zilikuwa za ujima ndiyo maana akina Butiku walimharibia mzee Nyerere mpaka akawa anaitwa Musa na mzee Haambiliki. Au Butiku amesahau jinsi alivyokuwa anapendelea watu wa kabila la kutoka Musoma ndiyo maana akina Warioba wakainukia. Enzi zile watu wa Musoma wakiitwa true Northerners. You had to come from true north to be given responsibilities especially sensitive ones kama jeshi, usalama wa taifa BOT n.k Kama hutoki huko hupewi cheo cha maana hata kidogo. Butiku amesahau hilo?
OK, unachukua kitu chenye ukweli na kuki-stretch to the limit. ni kweli kulikuwa na a cabal of northerners, aprticularly people from Mara (Butiku, Apiyo, Musuguri mpaka vijana wa enzi zile kina Matiko etc). Lakini hii impression unayoitoa hapa kwamba hawa watu walikuwa wameweka lockdown kwenye system si kweli. Na wala Nyerere hakuwa zezeta wa kuchaguliwa watu na Butiku to that extent. Maneno yako mwenyewe yanakusuta, umesema bila ya kuwa northerner mtu alikuwa hawezi kupata kazi za usalama wa taifa na jeshi, halafu hapo hapo umemtaja Kitine kama mkuu wa usalama, Hivi Kitine ni northerner yule? Si mtu wa nyanda za juu kusini yule? Na hata mkuu mwingine wa usalama zamani ambaye sasa yuko ubalozini NY, Dr. Augustine Phillip Mahiga, alishika hii post na ni mtu wa kutoka Iringa. Hivi Nyerere kama angekuwa mkabila kiasi hicho angemuachia Mwinyi achukue urais baada yake? Warioba aliteuliwa kuwa PM na nani kama si Mwinyi?
Nakubali Butiku, Apiyo na wazee fulani wa Kikurya/ Kijita/ Kizanaki walio roll na hii Ikulu/ Intelligece/ Armed Forces clique walikuwa na impunity ya ajabu, complete with their crazed sex parties kwa mzee Butiku ( ndiyo maana naona hii moral authority yake inakuwa tainted na hypocrisy na nostalgia to an extent) . But this movement is bigger than Butiku, kuna yule kichaa msemaovyo wa kimasai anayepiga mke wake na kuamini mke ni property mpaka leo, by the name of Mateo Qaresi, Qaresi is too real to engage is some political nostalgia. Na washukuru yule Zen Buddhist wa kuitwa Phillip Mangula ameamua kukaa kimya kwa kufuata Confucian principles zake za "silence is golden" kwa sababu yule ndiye anayejua mikakati yote ya chama na anapewa data na team yake mpaka leo.
Enzi zile hazikuwa kama leo ambapo nchi imebadilika kiteknolojia kwa hiyo huwezi ukategemea JK afanane na Nyerere au Mwinyi. Akitaka kufanana hivyo mnamtaka awe Dikteta? Jk anasoma alama za nyakati na anajua anachopaswa kufanya. Tanzania ya leo yule Prosper Mbena amabye ni Private Secretary wa Rais JK au kabla yake yule David Jairo hawawezi kuwa powerful kama alivyokuwa Butiku. Why? Kwa sababu mazingira ya leo siyo kama yale akina Nyerere. Jamani miaka hiyo Butiku ndiyo aliekuwa anawapa watu vyeo.Ukitakata kuukata upewe cheo lazima ukalambe miguu ya Butiku na akukubali. Muulizeni Mhe. Kitine alivyopanda kutoka kuwa Major kule chuo cha Monduli na kufikia cheo cha Mkurugenzi
Mkuu wa Usalama wa Taifa. Badala ya kufanya kazi cheo kikampanda kichwani akawa anatembeza ubabe na starehe tu. Siku zile Radio moja TRD, Magazeti mawili Daily News la Serikali na Uhuru/Mzalendo la CCM. Kwa hiyo upuuzi wao ukawa hauandikwi. Isipokuwa zilikuwa zinadumishwa fikra za Mwenyekiti wa CCM.
You not only missed the boat, you missed the entire monsoon season.
This is not about trying to Nyerereize Kikwete, Kikwete is cut from a different cloth, hawa wazee wanakemea blatant disregard for leadership principles na a clear lack of direction. Kikwete amekuwa a laughingstock kiasi cha kwamba hata sisi tulioamini kwamba Ali Hassan Mwinyi ndiye aliyekuwa rais lowest kabisa katika uongozi na hakutakuja kuwa na rais atakayemshinda kwa hilo, tumebadili mawazo sasa na tunaona Kikwete kachukua kombe hilo.
Tanzania ya leo haiwezi kurudi huko. Ninawaomba hao wazee watulie waandike vitabu na wale pensheni zao. Wakijiingiza kwenye uharakati wa siasa pensheni zao zitaliwa na madalali wa kisiasa ambao wako wengi siku hizi. Tanzania ya leo ni ya dotcom. Wawaachie akina Nnape, Masha,Serukamba, Vita Kawawa, Mnyika, Mbowe na kizazi cha akina JK na Lowasa ndiyo wawe wana kongamano kwa nia ya kuipeleka nchi mbele.
Mara unawataka wazee wasiseme, mara unawataka waandike vitabu - as if that is any different- yaani hueleweki unataka nini.
Hebu angalia wale wazee kwenye kongamano lile. They are all spent forces. Hawana jipya. Mimi ningefurahi kama UDSM na vyuo vingine wangewatumia wazee hao kama wahadhiri ili wawafundishe vijana uzoefu wao.
Mara wazee spent forces hawana jipya, mara UDSM na vyuo vingine viwatumie hao kama wahadhiri wawafundishe vijana uzoefu wao.
Hii schizophrenia inatoka wapi hii? Can you make up your mind?
Spent forces wasio na jipya wataenda kufundisha nini cha muhimu vyuoni?
Wahadhiri wanaoweza kufundisha vyuoni watakuwaje spent forces?