Kongamano la kibiashara Urusi na Tanzania jijini Dar es Salaam 2024

Are our So called experts Well equipped To deal with This?

And other Trade relationship with Foreign Partners?

It's a chess match .
 
Hapo us roho inauma

Kila superpower China, USA na Russia n.k anavutia maslahi yao upande wake, waziri wa Putin yupo Tanzania huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo Marekani muda huu kufuatilia Kilimo Kwanza ajenda ya Chakula ni Usalama
 
Kuna tatizo!?..akina bush wanachimba dhahabu tangu 1990s unyamwezini/sukuma na wanawaacha mashimo tu
 
Michikichi siyo miwa au mipapai,huchukua miaka kuanza kuzaa
 
Michikichi siyo miwa au mipapai,huchukua miaka kuanza kuzaa
Najuwa mkuu, lakini hata habari za maendeleo yake ziwe kimya kabisa?

Haya, hebu saidia wewe unaye juwa kinacho endelea na mradi huo:ni hekta ngapi zilipandwa na sasa zinasubiriwa tu zitakapo kuwa tayari Tanzania ianze kupata neema wanazo zipata akina Indonesia na Malaysia?

Viwanda navyo itabidi visubiri hadi hapo kila mmea utakapo anza kutoa mazao? Wananchi je, na wao wamejipanga vipi kufaidika na mradi huo, au maandalizi ni hadi hapo kila kitu kitakapokuwa tayari?

Mkuu, nakusihi wewe utuletee hapa mrejesho wa hali ilvyo huko Kigoma kuhusu zile kelele nyingi sana tulizo sikia wakati ule.
 
Urusi ina bidhaa gani za kuleta Africa? Zaidi Meli yao itakuwa inafanya ro-ro trip port to port!
 
Noted 🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
30 October 2024

TANZANIA KUNUFAIKA NA FURSA LUKUKI ZA URUSI / KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI LAZAA MATUNDA


View: https://m.youtube.com/watch?v=HYLXmm1Kp9E
Urusi au Belarus hapana, tutafute marafiki wengine lakini siyo hao.
 
Bado unaishi kwenye "Vita Baridi" mkuu 'John'?
Je, Unawafahamu vizuri Watu wa Urusi?
Uneshawahi kwenda na kuishi nchini Urusi au umewahi kuishi pamoja na jamii za Watu wa Urusi ?

Hata baadhi ya raia wa Urusi wenye akili timamu sawa sawa huamua kuikimbia Urusi au kuwakimbia Warusi wenzao na kwenda kuishi au kuwekeza miradi yao nje ya Urusi kwenye nchi ambazo Hakuna siasa za Itiikadi za Ujamaa/Ukomunisti.
 
Hakuna cha bure dunia hii,,,hata hao unaowataka wewe wakija lazima wawe na kitu cha kuwapa manufaa pia
 
Umeuliza maswali mengi yasiyo kuwa na msingi wowote.
Kama wewe umeishi nao na kuwa na tofauti nao, unadhani wengine wote wanayo hisia kama yako?

Hasa sielewi mantiki ya hayo uliyo eleza hapa. Kwani urusi hawakuwahi kuwa na msaada kwa watu wengine? Hukumbuki msaada wao ukombozi kusini mwa Afrika?
Mbona watu wengi tu wamesoma na hata kuoa/kuolewa Urusi? Wewe walikufanyia kitu gani?
 
Ukombozi gani huo huko Kusini mwa Afrika?
 
Hakuna siasa za Itiikadi za Ujamaa/Ukomunisti
Alaaa!
Nilikuwa sijakusoma hadi mwisho. Kumbe shida yako ni hii?

Wewe utakuwa bado kasumba imekujaa sana kichwani kama bado umeshikilia mambo kama haya.

Kumbe sikukosea nilipo kueleza kuwa bado unaisha kwenye enzi za zamani.

Sasa wewe huoni hapo hao wanaotafuta kuwekeza hawana ukomunist; au ukomunisti kwako ni kitu gani?
 
Kuna kikundi cha wachekeshaji wanakibwagizo chao wanakwambia PIKA BOM💣.

Hii ni fursa kubwa sana kwa Tanzania kukua kiuchumi.

Rai yangu kwa wanausalama waangazie kwa jicho la tatu ni athari hasi zipi tutazipata kwaushirikiano huu na namna gani wanaweza wakacheza nazo (sukuma kete) ili tusijikute centre ya mapambano, maana maslahi yanagonganishwa hapa.

Waswahili wanakwambia umegonganisha mabwana.
 
Nawafahamu vizuri Warusi, kwa jinsi ninavyofahamu, Warusi ambao wenye akili nzuri na timamu sawa sawa kabisa, KAMWE hawawezi kuja kuwekeza kwenye nchi kama Tanzania, kamwe haitatokea. Warusi wenye akili timamu sawa sawa kabisa huwa wanaenda kuwekeza kwenye nchi za Magharibi, kama vile Marekani au nchi washirika wake mfano: Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Canada, Australia, n.k. Fanya utafiti wako binafsi utakuja kukubaliana na Ukweli huu.
 
Wewe mtu unahitaji msaada mkubwa na akili za namna hii.
Hao "warusi wenye akili timamu", kama wewe siyo?

Hata hujui au hukumbuki hao hao wanalia hii leo kwa kuwekewa vikwazo na hao unao waabudu wewe?

Hata maana ya kuwekeza hujui? Kwenda kuwekeza kwenye timu ya mpira wa miguu unakulinganisha na kuwekeza mahali ambapo soko linainukia na uwekezajiwake bado ni nafuu kabisa, kama Tanzania?

Kama nilivyo eleza toka mwanzo. Tatizo lako ni kasumba tu! Umekariri prpaganda zilizo pitwa na wakati, kiasi kwamba inakuwia vigumu kuachana nazo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…