Kongamano la Kwanza la Kitaifa kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Ushiriki wa Wananchi katika Kuunda Dira ya Taifa

Kongamano la Kwanza la Kitaifa kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Ushiriki wa Wananchi katika Kuunda Dira ya Taifa

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Habarini Wanajamvi,

Leo, tunashuhudia tukio la muhimu la Kongamano La Kwanza La Kitaifa kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, likiendelea hivi sasa. Ni fursa adhimu kwa kila Mtanzania kushiriki katika kujenga mustakabali wa Taifa letu. Makamu wa Rais, Dr. Philip Mpango, anahudhuria kama mgeni rasmi, akisisitiza umuhimu wa kila mmoja wetu kutoa mchango wake.

Dira ya 2050 siyo tu ramani ya maendeleo yetu, bali ni mwongozo wa kufikia Tanzania tunayoitamani. Swali la msingi linalojitokeza ni: Je, tunataka Tanzania iweje ifikapo mwaka 2050? Je, ni nini kipaumbele chetu kama Taifa katika elimu, afya, uchumi, na utawala bora?

Tunapaswa kuchukua nafasi hii kutoa maoni yetu, kushiriki katika mijadala, na kutoa mapendekezo yenye tija. Tume ya Mipango imetoa wito kwa kila mmoja wetu kushiriki kikamilifu. Hii ni nafasi ya kipekee kwa wananchi kuelezea matarajio yao na kuchangia katika kuiandaa Dira itakayokidhi mahitaji ya kila Mtanzania.

Je, ni vipi tunaweza kuhakikisha ushiriki mpana na wenye tija kutoka kwa wananchi wa kila kona ya nchi yetu?

Je, ni mbinu gani zinazoweza kutumika kuwafikia na kuwashirikisha wananchi ambao hawajapata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika kongamano hili?

Je, ni masuala gani muhimu yanayopaswa kupewa kipaumbele katika maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050?

Nawaalika wanajamvi kutoa maoni yenu, kushiriki katika kujenga hoja, na kuchangia katika mjadala huu muhimu. Kumbuka, sauti yako ni muhimu katika kuijenga Tanzania ya kesho.

KONGAMANO (08/06/2024: Nkuruma Hall) 👇


UPDATES:

PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAISI WA TANZANIA
Mwaka huu 2024 Umoja wa Mataifa umeanza mchakato wa kuiondoa nchi yetu kwenye kundi masikini sana duniani (least developed countries) kwa viashiria mahususi vya maendeleo.

Hli ya uhitaji wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka 56% mwaka 2000 hadi 26.4% mwaka 2018. Umasikini wa chakula umepungua kutoka 19% mwaka 200 hadi 8% mwaka 2018.

Upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya afya na umeongezeka kutoka 64% mwaka 2015 hadi takribani 80% mwaka 2022.

Kutokana na changamoto za mabadiliko, tunaweza kupoteza 1% -2@ ya pato la taifa ifikapo mwaka 2030. Aidha, katika wakati dunia inahamia kwenye matumizi ya nishatisafi ya kupikia, yaani umeme na gesi, ni 7.3% tu ya Watanzania wanatumia nishati hiyo mwaka 2022/23. Wananchi wetu wengi bado wanatumia kuni na mkaa kupikia na wanapata athari nyingi za magonjwa, hasa ya mfumo wa hewa, macho na kutumia muda mrefu kutafuta kuni.

Ukuaji wa matumizi ya teknolojia nao bado ni mdogo, hali inayozorotesha mabadiliko makubwa ya kiuchumi na ukuaji wa tija. Mathalani, katika mwaka 2016 – 2021, kasi ya mabadiliko ya kimuundo (structural change across sectors) ilishuka kutoka ukuaji wa 2.5% - %-0.5

Kwa upande watija, ukiangalia annualized productivity growth katika sekta ya kilino ambayo ndiyo inaajiri 61% ya Watanzania ilipungua kutoka 1.1% katika kipindi cha 2006 hadi 2014 hadi 0.7% katika kipindi cha 2014 – 21.

Ndugu washiriki, sasa ningependa kuachichia kongamano hili mambo matano ya kutafakuri katika zoezi hili la dira tulilolianza.

Ninawasihi wanazuoni na wananchi wayachukue mawazo haya kuwa ni kuchokoza tu majadiliano. Kwahivyo naomba washiriki wa kongamano wawe huru kabisa kuleta mitazamo na mawazo mapya itakayofaa zaidi kuingia kwenye dira mpya.

Jambo la kwanza. Dira ya 2050 inapaswa iwe ni ya vijana zaidi na kwa ajili ya vijana. Na sababu yake ni kwamba Sensa ya 2022 imebainisha kuwa 77% ni vijana na Watoto kati ya miaka 0-35, huku kundi la vijana wa miaka 15-35 wakiwa ni 34.5%. Kwa maana hiyo, Dira ya 2050 ni lazima nitambue mahitaji yao na ibebe matamanio ya kundi hilo kubwa la watu wetu.

Dira ibainishe fursa na changamoto za muundo na mwenendo huo wa idadi ya watu katika taifa letu. Sasa, fursa hizo ni pamoja na namna bora ya kutumia nguvu kazi ya vijana kuharakosha maendeleo au kwa lugha ya kigeni, harnessing the demographic dividend.

Jambo la pili. Dira ya 2050 ni muhimu ijengwe juu ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Dira inayofikia ukomo kwa kuyaimarisha, yaani consolidate the gains, na kutumia kama nyenzo ya kuongeza kasi ya mabadiliko makubwa.

Aidha, ni muhimu Dira ibainishe fursa za nchi yetu kwa kuzingatia mahitaji ya ndani na je ya nchi. Na eneo la kuangalia kwajicho la karibu ni rasilimaliza madini tulizo nazo kama taifa. Itakuwa vema uvunaji wa madini na hususani madini ya kimkakati (nickel, lithium, helium, uranium, cobalt n.k) upangwe kwa umakini mkubwa ili kuweza kunufaisha zaidi taifa kwa kuweka viwanda vya uchenjuaji wa madini hayo.

Jambo la tatu. Dira ya 2050 itapaswa kubainisha changamoto za ndani na za nje pamoja na zile za zamani zinazoibukia ambazo ni ni kikwazo kikubwa kwa nchi yetu katika kupata maendeleo haraka. Na hapa itakuwa vyema yakibainishwa kwa ukweli na uwazi. Na changamoto moja kubwa ninayoiona inahusu mapungufu katika utawala bora na uwajibikaji katika ngazi mbalimbali na pia changamoto za kiutamaduni na kimaadili.​

PROF. ISSA SHIVJI
Ni faraja kubwa kwangu kuwa kkongamano hili linafanyika ukumbi wa Nkuruma.Ingawa mambo yamebadilika siyo kama zamani…

Baada ya hotuba ya Makamu wa Rais, sijui nisema nini kwasababu amezungumza mengi niliyotaka kuzungumza.

Nitafafanua dhana ya dira na kutofautisha maneneo mengine ambayo tumezoea kuyatumia. Dira inaongoza katika kupanga mipango, ingawa dira yenyewe siyo mipango. Pia dira siyo malengo. Mipango ndiyo inakuwa na malengo.

Dira ni nini? Kwa maoni yangu, nadhani na Makamu wa Rais amegusia hili, dira ni maono (vision) ya nchi au ya taifa, au ya jamii ya watu katika ujumla wao. Ni maono ya aina ya nchi wanayotaka kujenga.

Kama nilivyosema, dira haina muda maalumu kama mipango. Dira inashawishi watu, inawa-inspire watu. Dira inawapa matumaini watu. Dira ndiyo inaleta watu woote kwa pamoja kwakuwa wanakubaliana aina ya nchi wanayotaka kujenga.

Dira ni kama follow star inayowasaidia mabaharia kufika kwemye destination. Inaongoza kuelekea mwisho wa safari yako. Sifa tatu za dira ni pamoja na, dira inakuwa ya taifa kwasababu inazungumzia dhamira ya watu. Pili, dira haina muda maalum. Huwezi kusema kuwa itachukuwa muda gani kujenga nchi yako. Tatu, nyuma ya dira kuna mtazamo wa falsafa. Falsafa siyo taaluma. Kila mwanadamu ni mwanafalsafa. Kwasababu falsafa ni fikra juu ya maisha ya sasa nay a baadaye.

Unaweza pia kusoma Thread 'Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ni Juni 8, 2024'
 
Ile ya National Development Vision 2025 wamewahi kufanya evaluation au bora liende?
 
Katumwa Tena Aliyekuwa Kwenye Mei Mosi Arusha Akasoma Hotuba Akajiondokea
 
Nyie pigen hela tu Tanzania tangu lin mwananchi akasikilizwa
Mmh. Anyway, ni kweli kwamba kumekuwa na changamoto za ushirikishwaji wa wananchi katika mambo muhimu ya kitaifa. Hata hivyo, nataka nikuhakikishie kuwa mimi sio sehemu ya waandaaji wa kongamano hili. Mimi ni mwananchi mwenzako, mwenye shauku kubwa ya kuona maendeleo na mabadiliko chanya katika nchi yetu, ikiwemo hili la ushirikishwaji wa wananchi.

Ninaamini kwamba kila mmoja wetu ana nafasi na sauti katika kujenga mustakabali wa Tanzania. Ushirikishwaji wa wananchi ni nguzo muhimu katika demokrasia yetu, na ni haki yetu kutoa maoni na kushiriki katika mijadala inayogusa hatma ya Taifa letu.

Kongamano hili ni fursa ya kipekee kwa sisi wananchi kutoa maoni yetu na kuchangia katika maandalizi ya dira itakayotuongoza kwa miaka ijayo. Ni muhimu kwa waandaaji kusikiliza sauti za wananchi na kuzingatia maoni yao katika kufikia maamuzi.

Ninakuhimiza na kuwaalika wenzetu wote kushiriki kwa njia mbalimbali, iwe ni kwa kuhudhuria kongamano, kutoa maoni kupitia mitandao ya kijamii, au hata kujadili na majirani zetu. Kila sauti ina thamani, na kila mchango unaweza kuleta tofauti.​
 
Kama Tuliwaambia wasiuze bandari kwa DP World wakatudharau sidhani kama wako serious kwenye hili la kutaka maoni yetu.

Wao waendelee kukopa tu wajukuu watalipa
 
Kama Tuliwaambia wasiuze bandari kwa DP World wakatudharau sidhani kama wako serious kwenye hili la kutaka maoni yetu.

Wao waendelee kukopa tu wajukuu watalipa
🤔 Point📌, ila wacha tushiriki maoni yetu ili yasipofatwa tuweze kusema hayajafatwa kuliko kukaa kimya tu.​
 
Kuna mama katibu wa semakafu kutoka jukwaa la wanaume dah kafoka hatari kuhusu usawa wa kijinsia hadi nikaona nibadili channel
 
Back
Top Bottom