Kongamano la uwekezaji katika sekta ya misitu kufanyika Iringa Novemba 10 - 12

Kongamano la uwekezaji katika sekta ya misitu kufanyika Iringa Novemba 10 - 12

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Posts
203
Reaction score
83
Mkoa wa Iringa ambao una miliki 40% ya misitu ya nchini Tanzania unatarajiwa kufanya Kongamano kubwa la wawekezaji na wadau wa sekta ya misitu tarehe 10 hadi 12 Novemba 2021. Akizindua maandalizi ya Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Queen Sendiga alisema ‘’ Mkoa wa Iringa ni kinara wa sekta ya misitu, na sasa Serikali ya Mkoa wa Iringa baada ya kuzindua mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Iringa mwanzoni mwa mwaka 2021, sasa tunaleta kwenu kongamano hili la uwekezaji katika sekta ya misitu ambalo litaenda sambamba na maonesho ya sekta ya misitu na pia kongamano la wadau wa sekta hii’’.

Aliendelea kusema ‘’ pamoja na Mkoa wa Iringa kuwa kinara wa Sekta ya misitu lakini bado kuna fursa pana za uwekezaji na uanzishaji wa biasahra au huduma kwenye sekta ya misitu, Wilaya zote za Mkoa wa Iringa zimetenga aridhi kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya misitu hivyo Twenzetu Iringa, Misitu inalipa , Wekeza Sasa.’’

Alimalizia kwa kusema tunatarajia Waziri Mkuu Mh Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano hili la Uwekezaji katika sekta ya misitu. Kujisajili kwa ajili ya kongamano hili bonyeza link hii Forestry Investment Forum | Iringa.

AVvXsEjK8L7akNf9d-OMsv9yrZ8HpWEgEA2e0S9jJhgLMKBGPC9EH3dlai5w9yY1YjLk0gKx49bmRAVsER-T4bIeLqEX4-nu8LloEngUOZUFEuJZKfTrCEUQg-1MFe7B6YyeRFTPgJrzYAxzupRJ07655AH4lVDg-eMvXgEpRxzG-_k6S8CgJgWuHWQ=s16000

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Queen Sendiga akizungumza wakati wa uzinduzi wa maandalizi ya kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya misitu.

AVvXsEhxUgNTmOOGsxogNfw9a05QK4wUaKlJ1SMUm-z4X0dXsJ-d5Mrm7aDMnnn-BI475Bio049mM74C4-RqWiVqFAHJaxpNeqp6edD9P0Rnz6FxlRSrQYe69ImL697wDG8YGyQt5Z-ZZHRFLVVlyWEH-ltfxa-8WDMy4IzufvJq63T2LhqKVTSaNuo=w640-h478
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Queen Sendiga akizungumza baada wa kuzindua maandalizi ya kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya misitu.

Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh Saady Mtambule , Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Mohamed Moyo na kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mh Peres Magiri
 
MAKONGAMANO ni vyanzo vya upigaji wa fedha za umma. Awamu ya tano hayakuwepo sasa yamezaliwa upya
 
Nadhani itakuwa mara ya kwanza wadau wa misitu kufanya hii kitu, ngoja tuone wanakuja na kitu gani then tutajua kama wameona fulsa ya kupiga hela au ni janja janja flani hivi!.
 
Back
Top Bottom