Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro wa Sekta za Mifugo, Kilimo na Usafirishaji

Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro wa Sekta za Mifugo, Kilimo na Usafirishaji

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
IMG-20240823-WA0038.jpg

Kongamano la Wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro wa Sekta za Mifugo, Kilimo na Usafirishaji limefanyika kwa mafanikio katika mji wa Moroni.

Katika kongamano hilo lililofunguliwa rasmi na Gavana wa Kisiwa cha Ngazidja, Mze Mohamed Ibrahim, wafanyabiashara wa Tanzania walikutana na wenzao wa Comoro na kufanikiwa kubaini fursa na mahitaji ya bidhaa za mifugo na kilimo hususan nyama ya ng’ombe, mbuzi, kuku, matunda, mbogamboga na nafaka.

Akifungua kongamano hilo, Gavana Mze alibainisha maeneo kadhaa yanayohitaji kufanyiwa kazi ili biashara baina ya visiwa hivyo iweze kushamiri na kueleza kuwa Comoro haihitaji kuagiza bidhaa toka nchi za mbali ilhali zinaweza kupatikana kwa ubora ule ule toka kwa ndugu zao wa Tanzania.

Awali akiwakaribisha Wafanyabiashara hao Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe. Saidi Yakubu aliwaeleza kuwa biashara baina ya nchi hizo mbili imekuwa ikishamiri na kwa takwimu zilizopo takriban bidhaa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 148 ziliuzwa nchini Comoro toka Tanzania kwa mwaka 2023.

IMG-20240823-WA0037.jpg

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano baina ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), Jukwaa la Sekta Binafsi ( TPSF), Umoja wa Wafugaji, Wakulima na Wavuvi Comoro, Benki ya Exim Comoro na kuhudhuriwa na takriban wafanyabiashara 120 toka nchi hizo mbili.

Katika maelezo yake, Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka TIC aliwaeleza wafanyabiashara hao vivutio mbali mbali vya uwekezaji ambavyo mfanyabiashara toka Tanzania anapotaka kukuza biashara yake kwa lengo la kuuza nje ya nchi anapata TIC na pia mamlaka ya kukuza uuzaji bidhaa nje EPZA. Aidha kwa wafanyabiashara wa Comoro aliwaeleza pia vivutio wanavyoweza kupata kwa kuwekeza Tanzania.

Kongamano hilo pia lilikuwa na vikao kadhaa vya uwili ambapo wafanyabiashara waliweza kuelezana fursa za kibiashara zilizopo miongoni mwao na mashirika ya usafirishaji ya Air Tanzania na Precision Air pia walishiriki na kutoa maelezo ya bidhaa zao.

Wafanyabiashara wa Tanzania pia walitembezwa katika soko maarufu Comoro la VoloVolo na pia katika ranchi ndogo kushuhudia ufugaji unavyofanyika.

IMG-20240823-WA0034.jpg
IMG-20240823-WA0033.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240823-WA0039.jpg
    IMG-20240823-WA0039.jpg
    193.1 KB · Views: 2
  • IMG-20240823-WA0040.jpg
    IMG-20240823-WA0040.jpg
    133.4 KB · Views: 3
  • IMG-20240823-WA0041.jpg
    IMG-20240823-WA0041.jpg
    115.7 KB · Views: 2
  • IMG-20240823-WA0035.jpg
    IMG-20240823-WA0035.jpg
    183.4 KB · Views: 4
Hongereni sana, ili kuwa miongoni mwa washiriki wa hizi safari za kibiashara natakiwa nifuate utaratibu gani?.
 
Back
Top Bottom