Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Wadau hamjamboni nyote?
Taarifa kamili hapo chini:
Samaha Mufti wa Tanzania Dr. Abubakar Zubeir Ali Mbwana amewataka walimu wa Madrasa kote nchini kujiendeleza kielimu na kujifunza fani mbalimbali zitakazowawezesha kufanya kazi yao vyema katika huu wakati wa mabadiliko makubwa ya kiteknolojia, kijamii, kiuchumi na kisera kwenye nyanja mbalimbali.
Mufti ametoa wito huo alipofungua kongamano linalowajumuisha walimu zaidi ya elfu moja na mia tano linalofanyika kwenye msikiti wa Kichangani Magomeni jijini Dar es salaam.
Aidha Mufti ameipongeza sana taasisi ya Hai-atul Ulamaa, Tanzania Muslim Solidarty Trust Fund na Tanzania Islamic Centre na waratibu wote kwa kuandandaa kongamano hilo kubwa.
Wahadhiri kwenye kongamano hili ni pamoja na Alhaj Mwalimu Juma Nchia, Dr. Kassim Nuruddin Hussein, Sheikh Shams Elmi kutoka Dhinnuurain, Dr. Pazi, Mhandisi Haji Mrisho, Kocha Mohammed Basanga, Hajjat Bi Mwanafumo Mwinjuma na Sheikh Muharrami Mziwanda.
Waratibu wa Kongamano hilo wanaongozwa na Alhaj Juma Nchia
Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa Mufti
Jumapili 7.7.2024
Magomeni - Dar es salaam