Rusumo one
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 3,458
- 4,283
Ugumu upo wapi mkuu?Hahaahaaaa.....hilo la Police kuungana na TISS gumu sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ugumu upo wapi mkuu?Hahaahaaaa.....hilo la Police kuungana na TISS gumu sana
Ngoja niwaze na mie! Hivi hawa WMA nao sijui wafutwe au waunganishwe unganishwe tu huko huko!!!!
Kweli jaman vibaka na wqbakaji nao waunganishe utendaji wao ,mabaa maid na mchangu doa nao wawe taasisi moja yqqni sasa waajiriwe machangudoa tu kwenye hizi local bar!hata waganga na wachawi pia wawe idara moja chini ya waziri wa ushirikina
Hapana. Zisiunganishwe ila majukumu yanayofanywa na hizi taasisi kwa pamoja ndio yawekwe kwenye taasisi moja(TFDA au Pharmacy Council).
Hii hoja ya kuweka majukumu yaliyokuwa yanafanywa na taasisi zaidi ya moja kwenye taasisi moja, naiunga mkono. Ila siungi mkono mambo kufanywa kisiasa bila kitaalamu.
Kwa muda mrefu sana, taasisi mbalimbali za kitaaluma zimeanzishwa kwa kukopi kutoka kwa wenzetu walioendelea mfano US wana FDA (Food and Drugs Authority).
Ukiangalia majukumu ya FDA ni kudhibiti Chakula na Dawa, japo kina majukumu mengine mengi inayafanya, lengo ni kuimarisha afya ya binadamu ndio maana Chakula na dawa vipo sambamba.
Hapa kwetu wanataka kutenganisha Chakula na Dawa(vitu ambayo kwa pamoja ni kuhusu afya ya binadamu), sikubaliani. Mambo yote yanayohusiana na Afya ya binadamu viwe sehemu moja(yafanywe na taasisi moja).
Hapa lengo ni kurahisisha utoaji huduma kwa jamii jambo ambalo ni zuri wasiweke majukumu yanayoendana katika taasis tofauti.
Kuna suala la kusajili majengo(Premisses registration) ambalo linaelekezwa TBS na kuna suala la kibali cha biashara ( business permit) ambalo lipo TFDA, haya mambo yanatakiwa yakae sehemu moja(TFDA). Anayesajili majengo ya biashara ndio atoe na kibali cha biashara.
Pharmacy Council isichanganywe na taasisi nyingine bali majukumu ambayo ilikuwa inayafanya halafu yanafanywa na taasisi nyingine yahamishiwe ama Pharmacy Council au taasisi hiyo. Pharmacy Council iendelee kudhibiti taaluma ya Pharmacy na mambo yote yanayohusiana na taaluma.
Mambo yasifanywe kisiasa, itakuwa kla siku tunabadilishana sheria pasipo na kusonga kimaendeleo.
Najua bas!nimechanganyikiwa kimtindo ghafla tu maichukia nchi yangu kuliko chochote kile bas kila neno naliona adui kwangu yaani nimedata kiaina!Unaandika nini mkuu?
wote wanaregulate madawaBara
Na TFDA wangeiunganisha na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).
hapa ipo kazi sana,Kwani mifuko ya kijamii ilipounganishwa wafanyakazi wa taasisi hizo walipelekwa/walibaki/walitawanywa wapi?
Hebu ulizia (wataalamu njooni) kwa wajuvi humu jamvini ili uni tag na mimi nipate mwanga/uelewa.