Kongole Mkuu wa Wilaya Petro Magoti

Kongole Mkuu wa Wilaya Petro Magoti

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,150
Reaction score
3,225
Najivunia sana kijana Petro Magoti aliyeteuliwa siku za karibuni kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Natamani wakuu wote wa wilaya wangeiga namna na jinsi anavyotenda na kuwajibika katika nafasi yake.
Kwanza anasimamia usalama wa watu wake, pili anafatilia miradi katika wilaya yake (anaingia field mwenyewe) tatu anasimamia nidhamu na malezi ya jamii, anatangaza vivutio vya utalii vilivyopo wilayani kwake.

Amenifurahisha zaidi alipoamua kwenda kuwatembelea wajasiriamali wa Kisarawe katika maonyesho ya sababa na kutangaza bidhaa zao yeye mwenyewe na kuwaahid kuwapa support Ili wafike mbali.

Kubwa zaidi ameonyesha njia kwa kuchangia mifuko ya saruji pale msikitini Ili mabweni yajengwe watoto wafundishwe Huku wakipata makazi standard yenye usalama wa hali ya juu.

DCs wote wa Tanzania mna la kujifunza kwa huyu bwana
 
Bado anahitaji ajifunze zaidi uongozi kwa vitendo na aache kutoa matamko kwa kukurupuka.

Labda huko mbeleni akijitahidi atakuwa wa mfano kwa sasa bado sana.
 
Najivunia sana kijana Petro Magoti aliyeteuliwa siku za karibuni kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe...
Nchi haihitaji viongozi aina ya Magoti wanaleta uchonganishi kwa wananchi dhidi ya serikali yao anafanya maigizo yasio na tija kiufupi mkeka ujao mtu wako hayumo ameonyesha udhaifu katika kuongoza!
 
Najivunia sana kijana Petro Magoti aliyeteuliwa siku za karibuni kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Natamani wakuu wote wa wilaya wangeiga namna na jinsi anavyotenda na kuwajibika katika nafasi yake...
Kuna watu wako Brain washed na Mlengo wa dini zao kiasi kwamba hata ikikutwa AK 47 ama bangi kwenye nyumba zao za Ibada wanakwambia usiende kuitoa nenda kwa Viongozi wao waeleze wakutee!

Ni kituko, nilichooona amefanya Bw.Mdogo Magoti ni ustaarabu wa 100% angekuwa DC mwingine lile tukio kichapo kwanza huyo Shekhe angeshapewa kesi ya Ugaidi.

Na kwa 100% kinachofanyika pale ni mafunzo ya Itikadi kali na kuandaa Vijana waende kujiunga Alishabaab nk nk huko Msumbiji tuache kufumbafumba maneno.

Ndugu zetu acheni hizo mambo, mwakani tu 2025 kinaweza ingia chumaa Ikulu hizo stori na makaburi yanaweza watia hatiani hao wahusika mbeleni hali ya usalama ikiwa tete.
 
Huku Kwetu kuna msikiti nimepita wanafundishana kwa sauti ya Chini Kuhusu Kodi Za Nchi za Kiislamu... Huwa kuna mzee anakujaga mara moja moja mafundisho yake huea ni ya itikadi kali sana. ni Arusha
 
WE
GSY2ZwAWwAAXivk.jpg
 
Uhaba wa viongozi bora unafanya anayejaribu aonekane kama ndiye anaweza.
 
Najiuliza hivi viongozi hawawezi kutekeleza majukumu yao ya kila siku bila kua na makamera na waandishi?
 
Huyu jamaa anajitahidi kwakweli natamani apande cheo awe RC
Hahhaaaa, ila watanzania bwana....sasa alishindwa nini kwenda kimya kimya mpaka ajitoe kwenye media, na kupiga picha magodoro, isitoshe akawavamia watu usiku wamejipumzikia 😄

Halafu huoni kuwa wakuu wa wilaya ya kisarawe wanapenda sana media! Japo siwataji kamanda wangu Chibolo 😄
 
Back
Top Bottom