Kongole Wananchi, Mafanikio Ya Namna Hii Hayajawahi Kufikiwa

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Habari njema kwa familia ya Yanga SC na mashabiki wake wote. Napenda kuwapongeza kwa juhudi yenu kubwa na mafanikio mkubwa mlipata katika mashindano ya CAF Confederation Cup, Ligi Kuu na Azam Sports Federation Cup. Ni wazi kuwa mlichapa kazi kwa bidii na kujitolea sana ili kufikia mafanikio haya.

Katika msimu mmoja tu wa soka mmeweza kutwaa LigiKUU
Kombe la ASFC na kutinga fainali ya
Kombe la Shirikisho Africa.

Hakuna klabu kutoka afrika mashariki imefanikiwa kufikia hatua hizi.

Mashindano haya yalikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa timu nyingine, lakini Yanga SC mliweza kushinda michezo yenu kwa uadilifu, nidhamu na kujituma mnapocheza uwanjani.

Mafanikio haya ni uthibitisho wa uwezo wenu mkubwa na uwezo wa kocha, wachezaji, uongozi na mashabiki kufanya kazi kwa pamoja.

Napenda kuwahakikishia kuwa mafanikio haya ni kichocheo kwa Yanga SC kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.

Tunawatakia kila la heri katika michuano inayofuata na tutawaunga mkono daima. Hongera tena kwa mafanikio yenu makubwa.
 
Well done utololo. You arr the real champion, mmeshinda mechi ya fainal tena kombe likiwa uwanjani mbele ya rais wa nchi yao....
Hutu tusheria twa hovyo hovyo eti goli la ugenini ni uchafu katika soka. Ndio maana fifa, Uefa wametufuta..
Nii muda sasa caf nao watufute maana tunasababisha kupatikana bingwa wa mchongo kama huyu US Alger
 
Ha!ha! Mnasahau kama mlikandwa dar
 
Na ili makolo wazidi kuumia na kuwa na wivu zaidi.... msimu ujao tunaingia hatua ya finali CAFCL
 
Ahsanteee...💚💛💚💛💚💛💚💛💛
 
Ha!ha! Mnasahau kama mlikandwa dar
We umewahi ona fainali inaamuliwa kwa aggregate? Halafu dar hakukuwa na fainal, fainali ilikuwa leo ndio maana kombe lilikuwepo uwanjani. Aliyeshinda leo ndio alistahili kombe
 
Kombe lipo wapi? Uto mbona kujieleza ni kwingi bila sababu ya maana.

ليس لديك القدرة على القتال معنا نحن العرب الجزائريين ، فأنت لست كذلك بعد.
 
Kama kulikuwa na ushindani mkubwa mbona wengine wameshuka daraja huko? Labda ushindani dhaifu.
 

HABIB HABIB KOMBE HAWATAKI KUONYESHAىسويويويوطنينينينطني[emoji196][emoji196][emoji196][emoji196]
 
Mafanikio ni kuchukua Kombe, tofauti na hapoo ni msindikizaji km wengine tyuuh, yaan huna tofauti na waliotolewa hatua ya awali, ni mlipishana Muda tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mafanikio ni kuchukua Kombe, tofauti na hapoo ni msindikizaji km wengine tyuuh, yaan huna tofauti na waliotolewa hatua ya awali, ni mlipishana Muda tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Una maanisha ZALAN FC aliyetolewa hatua ya awali ni sawa na SIMBA SC iliyotolewa hatua ya robo fainali..?
 
Una maanisha ZALAN FC aliyetolewa hatua ya awali ni sawa na SIMBA SC iliyotolewa hatua ya robo fainali..?
Sawa na Yanga piaa, mlipishana muda tyuuh
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sawa na Yanga piaa, mlipishana muda tyuuh
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ujajibu swali?

Yaani ZALAN FC ni sawa na SIMBA SC?

Maana wote wametolewa CAF...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…