Njaa
JF-Expert Member
- Dec 6, 2009
- 1,022
- 412
Habari zenu wakuu....
Nimekuwa na maumivu ya koo kwa muda fulani, maumivu sio makali ila huwa nahisi kama kuna kitu kinakwaruza na kuuma kiasi (kwa muda mrefu sasa). Tatizo hili hutokea mara kwa mara hasa ninapokaa chini kwa muda mrefu kuandika. Nimeenda kwa madaktari mara kadhaa na huwa naambiwa kuwa kuna inflammation (kuvimba). Nilipouliza sababu wakasema mara nyingi ni aleji au matumizi ya vitu baridi... Niliamua kuacha vitu baridi ila bado hali hii hujitokeza...
Siku za hivi karibuni nimekuwa nikitoa vitu vya ajabu kooni, vinakuwa kama vipande vya ugali (saizi ya punje za mahindi) vyenye harufu mbaya sana, wakati mwingine nikikohoa tu vinatoka. Nilipewa dawa vikapungua......, Wiki hii nilihisi kuna kitu kinakwama kooni, nikaamua kuingiza vidole na kutoa hayo maugali kisha nikajisikia vizuri kabisa! Ila inaniogopesha sana ingawa mtu fulani akaniambia ni vitu vya kawaida......
Naomba ushauri na uzoefu wa hili? Je ni dalili ya nini? Mbona madaktari wanalichukulia poa? Ikiwezekan ni-PM
Nawakilisha