Koo langu - Msaada please

Koo langu - Msaada please

Njaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2009
Posts
1,022
Reaction score
412
Habari zenu wakuu....

Nimekuwa na maumivu ya koo kwa muda fulani, maumivu sio makali ila huwa nahisi kama kuna kitu kinakwaruza na kuuma kiasi (kwa muda mrefu sasa). Tatizo hili hutokea mara kwa mara hasa ninapokaa chini kwa muda mrefu kuandika. Nimeenda kwa madaktari mara kadhaa na huwa naambiwa kuwa kuna inflammation (kuvimba). Nilipouliza sababu wakasema mara nyingi ni aleji au matumizi ya vitu baridi... Niliamua kuacha vitu baridi ila bado hali hii hujitokeza...

Siku za hivi karibuni nimekuwa nikitoa vitu vya ajabu kooni, vinakuwa kama vipande vya ugali (saizi ya punje za mahindi) vyenye harufu mbaya sana, wakati mwingine nikikohoa tu vinatoka. Nilipewa dawa vikapungua......, Wiki hii nilihisi kuna kitu kinakwama kooni, nikaamua kuingiza vidole na kutoa hayo maugali kisha nikajisikia vizuri kabisa! Ila inaniogopesha sana ingawa mtu fulani akaniambia ni vitu vya kawaida......

Naomba ushauri na uzoefu wa hili? Je ni dalili ya nini? Mbona madaktari wanalichukulia poa? Ikiwezekan ni-PM

Nawakilisha
 
Mkuu.@Njaa Nenda hopitali kuu ya Muhimbili hapo Mjini Dar kama upo hapo.La kama haupo hapo nenda hospitali kubwa unapoishi wewe usidharau hayo matatizo yasije baadae yakawa ni makubwa uwe muangalifu.
 
Asante Jamadari, Madaktari wengi wa kawaida wanasema eti ni tatizo dogo. Wanadai ni allergy tu. Hivyo hawanipi referral ya kwenda ENT Muhimbili
 
Habari zenu wakuu....

Nimekuwa na maumivu ya koo kwa muda fulani, maumivu sio makali ila huwa nahisi kama kuna kitu kinakwaruza na kuuma kiasi (kwa muda mrefu sasa). Tatizo hili hutokea mara kwa mara hasa ninapokaa chini kwa muda mrefu kuandika. Nimeenda kwa madaktari mara kadhaa na huwa naambiwa kuwa kuna inflammation (kuvimba). Nilipouliza sababu wakasema mara nyingi ni aleji au matumizi ya vitu baridi... Niliamua kuacha vitu baridi ila bado hali hii hujitokeza...

Siku za hivi karibuni nimekuwa nikitoa vitu vya ajabu kooni, vinakuwa kama vipande vya ugali (saizi ya punje za mahindi) vyenye harufu mbaya sana, wakati mwingine nikikohoa tu vinatoka. Nilipewa dawa vikapungua......, Wiki hii nilihisi kuna kitu kinakwama kooni, nikaamua kuingiza vidole na kutoa hayo maugali kisha nikajisikia vizuri kabisa! Ila inaniogopesha sana ingawa mtu fulani akaniambia ni vitu vya kawaida......

Naomba ushauri na uzoefu wa hili? Je ni dalili ya nini? Mbona madaktari wanalichukulia poa? Ikiwezekan ni-PM

Nawakilisha
Sijawahi kusikia allergic reaction ya aina hio nadhani una mtatizo mengine au inflammation ya kawaida tu nakushauri uwahi hospitali uchukuliwe ultrasound ya koo lako na vipimo vya hayo maugali na TSH/FH4 ikiwezekana ili kuhakikisha hauna GOITER! Mueleze daktari kuhusiana na hayo "maugali" yanayotoka kooni!
 
Nenda ukafanye vipimo vikubwa ikiwezekana anza na kwa doc ngoma mwenge pale au muhimbili,
 
Imekuanza lini?na tezi zako zinavimba?na unapata maumivu ? Una umri gani?
 
Nenda haraka ENT muhimbili utasaidiwa kuna wataalamu safi pale wah usichelewe
 
Imekuanza lini?na tezi zako zinavimba?na unapata maumivu ? Una umri gani?

Nina miaka 32, tatizo hili lina miaka 3. Tezi zangu zinavimba ila sipati maumivu
 
Mkuupole, hyo hal imewahi kunipata mimi pia na harufu itokanayo na hvyo v2 ni mbaya mno .suluhsho ni hospital 2
 
pole mkuu nlivyoelewa hilo tatizo lako linaweza kuwa una
1. diverticulum... hili ni tatizo la misuli kulegea na kutengeneza mfuko wa pembeni (out pouching) kwa eneo kama hilo inaitwa zenker's diverticulum ... ndo maana vyakula vinaingia hapo badala ya kwenda tumboni
UCHUNGUZI na vpimo... kwanza wanafanya barrium swallow x-ray itaonyesha mfuko pili uanweza kufanya endoscope... nenda muhimbili.... kama ungekuwa mwanza ngekuona.
MATIBABU... ni upasuaji hakuna dawa ya kuondoa tatizo.
ingawa hili tatizo huwapta wazee but rarely kwa vijana pia
2. inaweza kuwa uvimbe kama tonsilitis,adanitis, jipu.. goitre au benign tumor not cancer usiogope... vyote hivi mpaka upasuaji fanya vile vipimo vya hapo juu
 
Asante mkuu...., Jamiiforums kuna kila watu
 
Back
Top Bottom