GE2025 Koplo Agness: Epukeni makundi yasiyo kuwa na faida kwenu

GE2025 Koplo Agness: Epukeni makundi yasiyo kuwa na faida kwenu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Wananchi wa Kijiji cha Makasini, Wilaya ya Kilindi, Mkoa wa Tanga, wametakiwa kuepuka makundi yasiyo na faida na badala yake kujikita katika shughuli na mienendo inayojenga tabia njema, hususan kuelekea siku ya kupiga kura.

1761373498917.png
Wito huo umetolewa, jana Oktoba 24, 2025, na Koplo wa Polisi Agness, alipokutana na wananchi katika eneo la Kijiji cha Makasini.

Soma: Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Mwaswengu awataka Wananchi Songe kudumisha Amani na Utulivu

Aidha, wananchi wamesisitizwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi, wakijenga mazingira ya amani na mshikamano ndani ya jamii, ili kuhakikisha kila mtu anahisi usalama katika maeneo yao.

1761373513296.png
 
Makundi? Itakuaje siku ya uchaguzi, mtajuaje usahihi wa makundi yatakayoenda kupiga kura kama si waandamanaji wale wanaogopewa?
 
Uzuri tumeruhusu wananchi wote wote watoke, wenye NIDA halali na za michongo, leseni halali na za michongo+ wenye vitambulisho vya kupigia kura hivyo siku hiyo na kuendelea ni show show. Mizinga ya nyuki imeandaliwa ya kutosha. Wahuni wanakamatwa wanafungiwa ndani ya chumba na nyuki.
 
Maandamano yasiyojulikana yamewatikisa vya kutosha
 
Nchi ina amani ya kutosha ila watekaji ndio wanavuruga amani
 
Back
Top Bottom