Kopo la kwanza, la pili, la tatu kageuka chatu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Hakika miaka imekwenda na kila mtu unapoangalia nyuma mengi yanakujia yakufurahisha na kuchekesha na mengine ya huzuni kukutoa machozi.

Taarifa ya habari ya Al Jazeera inaonyesha watu Marekani wameandamana na kuvamia kituo kimoja cha jeshi la Marekani wakitaka kuingia ndani kuangalia watu kutoka kwenye sayari mbali na dunia (outer space) ambao wao wanaamini wamehifadhiwa ndani ya kituo hicho.

Imebidi walinzi watumie nguvu na kutishia kutumia silaha na mbwa wakali kuwazuia waandamanaji hao kuvamia kituo hicho.

Miaka ya 1980 siku moja ghafla Dar es Salaam ilipigwa na taharuki habari zimeenea mji mzima kuwa kuna mtu aliyekuwa anaoga Buguruni ghafla akageuka chatu.

Chatu huyo akachukuliwa kuhifadhiwa kituo cha polisi cha Buguruni.

Ghafla askari kituoni hapo wakashtukia wamezingirwa na umma mkubwa wa watu wamekuja kushuhudia kumuona huyo, ‘’chatu mtu.’’

Hii iliwaletea usumbufu mkubwa kwanza askari pale kituoni na wapita njia wa Barabara ya Uhuru.

Kila muda unavyozidi kupita ndivyo watu walivyojazana wamekuja kuona maajabu ya mtu kugeuka chatu.

Ilibidi kituo kifungue milango yake hadi selo za mahabusi kuwaita baadhi ya watu ndani na kuwapitisha kila chumba wahakikishe wenyewe kuwa hakuna chatu hapo ili watu waamini waondoke na utulivu na amani irejee hapo kituoni.

Watu hufikiri na kufanya mambo kutokana na mazingira yao.

Kwa Mmarekani hili la Mmrekani kuwa yuko ‘’bathroom,’’ maji kutoka ‘’showers’’ au ndani ya ‘’bathtub,’’ kumgeuza mtu kuwa chatu ni jambo liko mbali sana wala halimpitii katika fikra yake.

Lakini kwa Mtanzania khasa wa Buguruni yuko kwenye msala wake uani choo cha shimo kinamkabili yuko na ndoo yake ya maji na kopo au kata anaoga na mlango wa choo gunia au bati fikra ya kuwa maji yale aliyoteka bomba la mtaani maji yale kumgeuza chatu si kitu cha ajabu sana.

Waafrika watu wa uchawi na mazingaombwe.

Wapiga mganda hawakuchelewa wakatunga nyimbo, ‘’Kopo la kwanza, kopo la pili, kopo la tatu kageuka chatu.’’

Basi siku ya tukio lile mimi niko Saigon akaja rafiki yangu Swahiba (Allah amrehemu), Maa Shaa Allah Mungu alimpa kipaji cha hali ya juu sana cha fasaha na uwezo wa kuchekesha na wala siongezi chumvi ni katika ‘’level’’ ya Bill Cosby, tofauti yeye kazaliwa Afrika.

Swahiba akaniuliza ile habari ukweli wake.
Nikamuhadithia toka mwanzo hadi mwisho na yeye anaitika kila sentensi yangu.

Nilipomaliza Swahiba akaangalia juu mbinguni huku kanyoosha kidole chake cha shahada, akaniambia, ‘’Unajua hili jua limekuwa kali sana.’’

Nadhani msomaji wangu umemwelewa Swahiba.
Mimi nilibakia kucheka tu.

Sijui hii ya hawa Wamarekani waandamanaji angesema nini.

Nina hakika mia kwa mia angesema, ‘’Hawa Wamarekani wapunguze hizi bangi na pombe zao.’’
 
Ilikuwa hivi hiyo story...
kuna mama alienda kwa mganga kutafuta dawa ya kumuewekea mumewe
sasa hiyo dawa ya kuoga alipoiweka ama kuna masharti alikosea au la
ndo mumewe kuoga tu akageuka chatu..

Sijui why hii story iliienea but ilienea sana

those days hakuna social media story za uwongo na kwweli zilikuwa nyingi

but kuna story ya kweli ilitokea ofisi za Tanesco head office
daktari kutoka zambia alikuwa foleni ya kulipia umeme akakaa nyuma ya mama
mwenye bonge la wowowo....mwisho dokta akatoa mshedede pale pale akapiga bao
ilikuwa big story na nyimbo za mdundiko zilitungwa...alishtakiwa sijui ikawaje
 
Hakika miaka imekwenda na kila mtu unapoangalia nyuma mengi yanakujia yakufurahisha na kucheksha na mengine ya huzuni kukutoa machozi.

Taarifa ya habari ya Al Jazeera inaonyesha watu Marekani wameandamana na kuvamia kituo kimoja cha jeshi la Marekani wakitaka kuingia ndani kuangalia watu kutoka kwenye sayari mbali na dunia (outer space) ambao wao wanaamini wamehifadhiwa ndani ya kituo hicho.

Imebidi walinzi watumie nguvu na kutishia kutumia silaha na mbwa wakali kuwazuia waandamanaji hao kuvamia kituo hicho.

Miaka ya 1980 siku moja ghafla Dar es Salaam ilipigwa na taharuki habari zimeenea mji mzima kuwa kuna mtu aliyekuwa anaoga Buguruni ghafla akageuka chatu.

Chatu huyo akachukuliwa kuhifadhiwa kituo cha polisi cha Buguruni.

Ghafla askari kituoni hapo wakashtukia wamazingirwa na umma mkubwa wa watu wamekuja kushuhudia kumuona huyo, ‘’chatu mtu.’’

Hii iliwaletea usumbufu mkubwa kwanza askari pale kituoni na wapita njia wa Barabara ya Uhuru.

Kila muda unavyozidi kupita ndivyo watu walivyojazana wamekuja kuona maajabu ya mtu kugeuka chatu.

Ilibidi kituo kifungue milango yake hadi selo za mahabusi kuwaita baadhi ya watu ndani na kuwapitisha kila chuma wahakikishe wenyewe kuwa hakuna chatu hapo ili watu waamini waondoke na utulivu na amani irejee hapo kituoni.

Watu hufikiri na kufanya mambo kutokana na mazingira yao.

Kwa Mmarekani hili la Mmrekani kuwa yuko ‘’bathroom,’’ maji kutoka ‘’showers’’ au ndani ya ‘’bathtub,’’ kumgeuza mtu kuwa chatu ni jambo liko mbali sana wala halimpitii katika fikra yake.

Lakini kwa Mtanzania khasa wa Buguruni yuko kwenye msala wake uani choo cha shimo kinamkabili yuko na ndoo yake ya maji na kopo au kata anaoga na mlango wa choo gunia au bati fikra ya kuwa maji yale aliyoteka bomba la mtaani maji yale kumgeuza chatu si kitu cha ajabu sana.

Waafrika watu wa uchawi na mazingaombwe.

Wapiga mganda hawakuchelewa wakatunga nyimbo, ‘’Kopo la kwanza, kopo la pili, kopo la tatu kageuka chatu.’’

Basi siku ya tukio lile mimi niko Saigon akaja rafiki yangu Swahiba (Allah amrehemu), Maa Shaa Allah Mungu alimpa kipaji cha hali ya juu sana cha fasaha na uwezo wa kuchekesha na wala siongezi chumvi ni katika ‘’level’’ ya Bill Cosby, tofauti yeye kazaliwa Afrika.

Swahiba akaniuliza ile habari ukweli wake.

Nikamuhadithia toka mwanzo hadi mwisho na yeye anaitika kila sentensi yangu.

Nilipomaliza Swahiba akaangalia juu mbinguni huku kanyoosha kidole chake cha shahada, akaniambia, ‘’Unajua hili jua limekuwa kali sana.’’

Nadhani msomaji wangu umemwelewa Swahiba.
Mimi nilibakia kucheka tu.

Sijui hii ya hawa Wamarekani waandamanaji angesema nini.

Nina hakika mia kwa mia angesema, ‘’Hawa Wamarekani wapunguze hizi bangi na pombe zao.’’

Sikumbuki exactly ilikuwa mwaka gani lakini kule Rombo kuliwahi enezwa uvumi kuwa kuna mtu aligeuka kuwa Tembo na kuanza kula migomba, na watu walifurika sana kwenye familia ya huyo mtu mamia kwa mamia....!!!
So sijui nianzishe uzi ili kama wapo wenye detail walete...
Mzee heshima yako!!
 
Ilikuwa hivi hiyo story...
kuna mama alienda kwa mganga kutafuta dawa ya kumuewekea mumewe
sasa hiyo dawa ya kuoga alipoiweka ama kuna masharti alikosea au la
ndo mumewe kuoga tu akageuka chatu..

Sijui why hii story iliienea but ilienea sana

those days hakuna social media story za uwongo na kwweli zilikuwa nyingi

but kuna story ya kweli ilitokea ofisi za Tanesco head office
daktari kutoka zambia alikuwa foleni ya kulipia umeme akakaa nyuma ya mama
mwenye bonge la wowowo....mwisho dokta akatoa mshedede pale pale akapiga bao
ilikuwa big story na nyimbo za mdundiko zilitungwa...alishtakiwa sijui ikawaje
What year was that! Nakumbuka nilikuwa shimo la udongo.
 
Nakumbuka kisa hiki kiliandamana na kile cha Sara Simbaulanga kuiba hela NBC.

Nilitembea kwa miguu toka Mabibo Kati (Makutano) mpaka Buguruni kituo cha Polisi kwenda kuangalia "Nyoka mtu". Nakumbuka Atilio Tagalile kwenye makala yake ya "Blah blah" alikiandika kisa hiki kwa utani mkubwa sana.
 
Nakumbuka mwaka 2016 mamia kwa maelfu ya watanzania walikusanyika pale kijiji cha ufuluma Mkoani Tabora kushuhudia gogo la mti lililokuwa limekatwa kunyanyuka na kusimama tena kwenye shina lake.

Siku chache baadae tukasikia Kule Tanga nyerere kaonekana kwenye mwembe.
 
Ilikuwa hivi hiyo story...
kuna mama alienda kwa mganga kutafuta dawa ya kumuewekea mumewe
sasa hiyo dawa ya kuoga alipoiweka ama kuna masharti alikosea au la
ndo mumewe kuoga tu akageuka chatu..

Sijui why hii story iliienea but ilienea sana

those days hakuna social media story za uwongo na kwweli zilikuwa nyingi

but kuna story ya kweli ilitokea ofisi za Tanesco head office
daktari kutoka zambia alikuwa foleni ya kulipia umeme akakaa nyuma ya mama
mwenye bonge la wowowo....mwisho dokta akatoa mshedede pale pale akapiga bao
ilikuwa big story na nyimbo za mdundiko zilitungwa...alishtakiwa sijui ikawaje
Mfadhahiko ndio ulianzia hapo,halafu baadae ndio wakatokea hawa kuitwa dungadunga,dungadunga wamejaa kibao kariako,ulaya na bara zima la marekani
Nalog off
 
Hiii habari imenifurahisha Sana ama kweli wabongo wanapenda uzushi Sana,vipi mnakumbuka 2011 Babu was loliondo?
Mpaka Mwendazake Jiwe alitekwa na Ile uvumi wa dawa ya UKIMWI na magonjwa sugu Kwa kikombe Cha jero na walimiminika kweli kumuungisha yule Mzee
Ambilikile Mwaisapile!

Wajinga hawataisha Labda bahari ikauke!
😂😂😂😂🔥🔥🔥🔥
 
Kidudu mtu watu wakaogopa kula kisamvu

1645125474082.png
 
Back
Top Bottom