Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hakika miaka imekwenda na kila mtu unapoangalia nyuma mengi yanakujia yakufurahisha na kuchekesha na mengine ya huzuni kukutoa machozi.
Taarifa ya habari ya Al Jazeera inaonyesha watu Marekani wameandamana na kuvamia kituo kimoja cha jeshi la Marekani wakitaka kuingia ndani kuangalia watu kutoka kwenye sayari mbali na dunia (outer space) ambao wao wanaamini wamehifadhiwa ndani ya kituo hicho.
Imebidi walinzi watumie nguvu na kutishia kutumia silaha na mbwa wakali kuwazuia waandamanaji hao kuvamia kituo hicho.
Miaka ya 1980 siku moja ghafla Dar es Salaam ilipigwa na taharuki habari zimeenea mji mzima kuwa kuna mtu aliyekuwa anaoga Buguruni ghafla akageuka chatu.
Chatu huyo akachukuliwa kuhifadhiwa kituo cha polisi cha Buguruni.
Ghafla askari kituoni hapo wakashtukia wamezingirwa na umma mkubwa wa watu wamekuja kushuhudia kumuona huyo, ‘’chatu mtu.’’
Hii iliwaletea usumbufu mkubwa kwanza askari pale kituoni na wapita njia wa Barabara ya Uhuru.
Kila muda unavyozidi kupita ndivyo watu walivyojazana wamekuja kuona maajabu ya mtu kugeuka chatu.
Ilibidi kituo kifungue milango yake hadi selo za mahabusi kuwaita baadhi ya watu ndani na kuwapitisha kila chumba wahakikishe wenyewe kuwa hakuna chatu hapo ili watu waamini waondoke na utulivu na amani irejee hapo kituoni.
Watu hufikiri na kufanya mambo kutokana na mazingira yao.
Kwa Mmarekani hili la Mmrekani kuwa yuko ‘’bathroom,’’ maji kutoka ‘’showers’’ au ndani ya ‘’bathtub,’’ kumgeuza mtu kuwa chatu ni jambo liko mbali sana wala halimpitii katika fikra yake.
Lakini kwa Mtanzania khasa wa Buguruni yuko kwenye msala wake uani choo cha shimo kinamkabili yuko na ndoo yake ya maji na kopo au kata anaoga na mlango wa choo gunia au bati fikra ya kuwa maji yale aliyoteka bomba la mtaani maji yale kumgeuza chatu si kitu cha ajabu sana.
Waafrika watu wa uchawi na mazingaombwe.
Wapiga mganda hawakuchelewa wakatunga nyimbo, ‘’Kopo la kwanza, kopo la pili, kopo la tatu kageuka chatu.’’
Basi siku ya tukio lile mimi niko Saigon akaja rafiki yangu Swahiba (Allah amrehemu), Maa Shaa Allah Mungu alimpa kipaji cha hali ya juu sana cha fasaha na uwezo wa kuchekesha na wala siongezi chumvi ni katika ‘’level’’ ya Bill Cosby, tofauti yeye kazaliwa Afrika.
Swahiba akaniuliza ile habari ukweli wake.
Nikamuhadithia toka mwanzo hadi mwisho na yeye anaitika kila sentensi yangu.
Nilipomaliza Swahiba akaangalia juu mbinguni huku kanyoosha kidole chake cha shahada, akaniambia, ‘’Unajua hili jua limekuwa kali sana.’’
Nadhani msomaji wangu umemwelewa Swahiba.
Mimi nilibakia kucheka tu.
Sijui hii ya hawa Wamarekani waandamanaji angesema nini.
Nina hakika mia kwa mia angesema, ‘’Hawa Wamarekani wapunguze hizi bangi na pombe zao.’’