HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
- Leo Jumamosi inatimia miaka 111 tangu kuzaliwa kwa mwasisi wa Korea Kaskazini, Kim Il Sung.
Siku ya kuzaliwa kwa Kim ni moja ya sikukuu muhimu zaidi za umma nchini Korea Kaskazini. Huenda Korea Kaskazini wakaitumia siku hii kuimarisha fahari ya nchi kama vile kutangaza mipango ya nyuklia na makombora ya nchi hiyo.
Jana Ijumaa Korea Kaskazini ilisema ilifanya jaribio la kwanza la kombora la kuvuka mabara la Hwasong-18 siku iliyotangulia. Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, alikuwepo.
Kombora hilo liliripotiwa kutumia fueli mango, inayowezesha urushaji kwa haraka.