Korea Kaskazini yaangusha mabaki ya kombora la masafa marefu ndani ya eneo la Japan

Majaribio wamefanya kwenye ardhi ya nchi nyingine, ni wazi huyu dogo husaka vita.
North korea hajarusha makombora kwenye ardhi ya japan na majaribio ya sasa hayajakiuka maadhimio ya UN kwa mujibu wa mkuu wa majeshi ya US yaliyopo korea kusini.

Kilichopo jina la bahari ndilo limewachanganya. Hii bahari wajapan wanaita bahari ya japan wakati wakorea(north na south) wanaita bahari ya mashariki.
Kuna kutokuelewana kati ya korea na japan kuhusu hii bahari.

Lakini makombora majaribio yamefanywa ndani ya mipaka ya korea kaskazini.
 
Majaribio wamefanya kwenye ardhi ya nchi nyingine, ni wazi huyu dogo husaka vita.
Hiyo ni kawaida Sana kwa mabaki kuangukia kwenye ardhi ya nchi nyingine
 

Inaitwa international geopolitics.... Lazima dunia ikae mkao wa balance fulani hivi, hairuhusiwi muwe ndugu nyote, inapaswa kanda fulani mnanuniana ili biashara na uchumi wa dunia uweze kutamalaki. Wahoji wabobezi kwenye haya mambo watakupa darasa, usisubiri hata siku moja dunia tukawa na amani pembe zote, na hata Marekani akianguka leo, lazima ataibuka mwingine wa kuendeleza chokochoko ulimwenguni.
 

Mbona asifanye kwake ndani, kwanini afanye kwenye eneo la bahari lenye utata baina yake na Japan kama sio ugomvi anaousaka, akirindima hayo makombora kwenye milima na mapori yake hakuna atakayehoji, au atupe kwenye eneo lake la bahari watamuacha kimya.

Hebu waza, itokee mimi na wewe tuna bifu na kaugomvi fulani, halafu nirushe ngumi kama ninayeelekeza kwenye pua lako ila nisitishe kabla kukugusa, niambie kama utakua na amani au wewe pia utajiandaa tuzipige.
 
Uchokozi waziwazi
 
Nimuhoji nani mimi ni mmoja Watanzania wachache tuliofika daraja linaloitenganisha China na Korea kaskazini sikuweza kupata visa ya NK kwa sababu nilikua na visa ya USA kitambo kwenye ile passport yangu ya zamani hapo Beijing ubalozi wa NK unaishia kwa Askari wa nje wanakwambia you Amerikani...
 

Itakua haukunielewa, hata kama umefika mpaka kwa Kim na mkanywa chai naye ila nilichokisema ndio uhalisia wa dunia, chukua muda wako kufuatilia chokochoko zote za dunia na zilivyokaa kiuchumi na kimahusiano utaelewa.
 
Itakua haukunielewa, hata kama umefika mpaka kwa Kim na mkanywa chai naye ila nilichokisema ndio uhalisia wa dunia, chukua muda wako kufuatilia chokochoko zote za dunia na zilivyokaa kiuchumi na kimahusiano utaelewa.
Ndio maana nimekwambia mimi siasa pamoja na kusikia huwa natumia muda wangu kwenda kujifunza mwenyewe sio kwa wapiga mbiu...
 
Hakuna mchi yoyoye inayozuiwa kutumia bahari ambayo ipo ndani ya mipaka yake.

Pili, utata uliopo kati ya korea na japan ni kuhusu jina la bahari tu na mipaka ya kila nchi inafahamika.


Hivyo, hakuna nchi yoyoye ambayo imewahi adhibiwa kwa kufanya makombora ya masafa mafupi na korea kaskazini hakuvunja resolution yoyote ya UN.
 

Haingii akilini ufanye majaribio ya makombora ya masafa marefu karibu na hasidi yako na pasipigwe makelele, kwa mfano Tanzana na Malawi huwa na kaugomvi fulani kuhusu jina la ziwa wanalochangia, sasa leo JWTZ waende kufanya majaribio ya makombora yenye uwezo wa kufika mji mkuu wa Malawi, wayafanyie hapo kwenye ziwa hilo......hata kama watakua wanapiga kwenye fukwe za Tanzania, lazima kutaibua yaliyofukiwa.

 
Ni wapi huko ambapo wamesema kuwa makombora ya sasa ni masafa marefu?

Korea Kaskazini amefanya majaribio ya makombora ya masafa mafupi ndani ya mipaka yake, ambalo hili hata mkuu wa majeshi ya us korea kusini amekiri kuwa ya kawaida na hakuna resolution yoyote iliyokiukwa.

Soma tena madai yako na nilichoandika utata kati ya korea na japani ni kuhusu JINA na sio MIPAKA kama mfano ulioutoa wa tz na malawi kuhusu ziwa nyasa.

Ndio maana kwenye bahari hiyo meli na ndege haziwezi pita maeneo ya mipaka ya North bila ruhusa yao na UN inatambua hilo.
 
North Korea does not have an embassy in the United States, so the visa must be obtained overseas ie.. at the DPRK Embassy in Beijing China
 
Alafu siku zote yule anayeanza chokochoko hua anakuja kupigwa vibaya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…