Korea Kaskazini yatamba kuwa miongoni mwa nchi chache ulimwenguni zenye uwezo wa kuitisha na kuiogofya Marekani

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
2,926
Reaction score
15,634
92619-untitled-design-15.jpg

Korea Kaskazini imetamba ktk jumanne ya wiki hii kuwa nchi hiyo ni moja ya nchi chache duniani zenye silaha za nyuklia na makombora yenye ubora wa hali ya juu. Ikaendelea kutamba kuwa nchi hiyo (Korea Kaskazini) ndio nchi pekee yaweza kuidindia Marekani kwa 'kuitikisa dunia' kupitia majaribio yake ya makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini ndani ya mwezi huu wa Januari, majaribio ambayo zBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa tamko kitambo la kuyazuia ingawa tamko hilo halifuatwi na Korea Kaskazini.

January 2022 imekuwa ni mwezi uliovunja rekodi kwani Korea kaskazini ilifanya mfululizo wa majaribio saba ya kurusha makombora, ambapo miongoni mwa makombora yaliyorushwa ni kombora jipya la hypersonic, lenye uwezo wa kusafiri zaidi ya mara kumi ya spidi ya sauti na pia lina uwezo mkubwa wa kufanya manuva likiwa kwenye spidi kali angani na hivyo kuepuka mifumo ya ulinzi wa anga la adui (kutodunguliwa).

Pia miongoni mwa makaribio hayo ilikuwa ni kurusha kombora la balistiki masafa ya kati, Hwasong-12, kombora lenye uwezo wa kushambulia ardhi ya Marekani iliyopo kwenye bahari ya Pasifiki.

"Katika Ulimwengu wa leo ambapo nchi nyingi zaendekeza kupoteza muda wao ktk kudili na Marekani kwa kuinyenyekea na kutii matakwa ya Marekani pasi kuhoji, utaipata nchi yetu pekee (Korea Kaskazini) kwenye hii sayari ya dunia ndio inaweza kuitikisa dunia kwa kurusha makombora yanayoweza kufika na kushambulia Marekani (US mainland)" Ilisema stetimenti ya wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini.

" Kuna nchi zaidi ya 200 ktk dunia hii, lakini ni nchi chache tu ndio zina mabomu ya atomiki (hydrogen bombs), makombora ya balistiki yenye uwezo wa kuvuka mabara (intercontinental ballistic missiles) na makombora ya haipasoniki (hypersonic missiles)" Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini ilifafanua zaidi.
 
Huyu bwana ana majivuno mengi sana[emoji16][emoji16], marekani huwa anamtazama tuu
 
Majivuno na vitambo ni tabia za madikteta wengi. Tabia nyingine ni ile ya kujipa majina wanayodhani yatatufanya tuwaone kama si binadamu wa kawaida.
 
Korea Kaskazini imetamba ktk jumanne ya wiki hii kuwa nchi hiyo ni moja ya nchi chache duniani zenye silaha za nyuklia na makombora yenye ubora wa hali ya juu. Ikaendelea kutamba kuwa nchi hiyo (Korea Kaskazini) ndio nchi pekee yaweza kuidindia Marekani kwa 'kuitikisa dunia' kupitia majaribio yake ya makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini ndani ya mwezi huu wa Januari, majaribio ambayo zBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa tamko kitambo la kuyazuia ingawa tamko hilo halifuatwi na Korea Kaskazini.

January 2022 imekuwa ni mwezi uliovunja rekodi kwani Korea kaskazini ilifanya mfululizo wa majaribio saba ya kurusha makombora, ambapo miongoni mwa makombora yaliyorushwa ni kombora jipya la hypersonic, lenye uwezo wa kusafiri zaidi ya mara kumi ya spidi ya sauti na pia lina uwezo mkubwa wa kufanya manuva likiwa kwenye spidi kali angani na hivyo kuepuka mifumo ya ulinzi wa anga la adui (kutodunguliwa).

Pia miongoni mwa makaribio hayo ilikuwa ni kurusha kombora la balistiki masafa ya kati, Hwasong-12, kombora lenye uwezo wa kushambulia ardhi ya Marekani iliyopo kwenye bahari ya Pasifiki.

"Katika Ulimwengu wa leo ambapo nchi nyingi zaendekeza kupoteza muda wao ktk kudili na Marekani kwa kuinyenyekea na kutii matakwa ya Marekani pasi kuhoji, utaipata nchi yetu pekee (Korea Kaskazini) kwenye hii sayari ya dunia ndio inaweza kuitikisa dunia kwa kurusha makombora yanayoweza kufika na kushambulia Marekani (US mainland)" Ilisema stetimenti ya wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini.

" Kuna nchi zaidi ya 200 ktk dunia hii, lakini ni nchi chache tu ndio zina mabomu ya atomiki (hydrogen bombs), makombora ya balistiki yenye uwezo wa kuvuka mabara (intercontinental ballistic missiles) na makombora ya haipasoniki (hypersonic missiles)" Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini ilifafanua zaidi.
Destruction cannot be positive at all.
 
Back
Top Bottom