Korea Kusini, Kaskazini wapiga Selfie, Lebanon wakataa kupanda basi moja na Israel

BigBro

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
3,585
Reaction score
11,601


Lee Eun-ju wa Korea Kusini (kulia) na Hong Un-jong wa Kaskazini walipiga picha wakiwa wametabasamu wakati wa mazoezi kabla ya kuanza kwa michezo hiyo. Picha hii imekuwa gumzo kubwa kwenye mitandao duniani.

Lee (kushoto) Miaka 17 anashiriki kwa mara ya kwanza michezo hii.

Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa Korea Kusini na Korea Kaskazini ambao ni ndugu wanaozungumza lugha moja wenye uhasama wa miaka, timu ya Olimpiki ya Lebanon imekataa kupanda basi moja na wanamichezo wa Israel hali iliyopelekea kutafutiwa basi jingine.

Kama kawaida USA Baby (Kwa mujinu wa Nyani Ngabu) Marekani inaongoza kwenye medali.

Source: Daily Mail
 
mmeshikilia tu namba ila ngoja mchina aje awapite hamtaamini
 
Ubaya wa China ni kwamba kila mchezo wamo.. ! So obviously wataongoza kwa medalist tu.. !
 
Tanzania ingepigania mchezo wa bao la jadi labda tungeambulia tumedali tumoja.
 
Tanzania ingepigania mchezo wa bao la jadi labda tungeambulia tumedali tumoja.
Michezo fulani imekaa kitamaduni zaidi na inawabeba kweli akina fulani. Wala sio ishu sana kukosa medali, muhimu ni kutengeza 'industry' imara hapa nyumbani
 
ni jambo zuri lakn hapa nasubir neno moja toka kwa kale karais kakibonge ka north korea.
 
Mbona huyo binti wa korea haonekani kama anatoka nchi fukara?
 
Nasikia kuna Machangu wa Kitanzania huko China wanafanya vzr, angalau hao wanatutoa kimasomaso.
 
Sisi. Kuna mambo yetu sisi. We tuache tu
 
Kwanza baadhi ya michezo sisi haipo kabisa kwenye Nchi Yetu
 
wazee wa vipedo huwa hawana msamiati wa kusamehe
 
Kama kawaida USA Baby (Kwa mujinu wa Nyani Ngabu) Marekani inaongoza kwenye medali.

That's right.

Na baada ya mashindano kuisha tutakuwa tumekomba medali nyingi kushinda mataifa mengine yote yaloshiriki.





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…