Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Mkuu mbona umefafanua vizuri tu, huyu anataka kupotosha members kimaksudi - point zako ziko valid kwa upande wa Tanzania vile vile na Kenya - Tatizo kubwa letu Wafrica ni kutaka kujikweza wakati mambo madogo yanatushinda, unawezaje kujidai kwamba nchi yako inataka kuwa na viwanda vikubwa vya kuhunda magari kuliko vya mji wa Detroit Marekani, si hilo tu wanakwenda mbali zaidi kwa kudai watajenga viwanda vya HiTech kushindana na vya Silcon Valley!!! Ndoto tu za mchana.
Badala ya kujikita kujenga vyuo vya Ufundi vyenye adhi kila mkoa ikiwezekana, sisi tunakimbilia kujenga White Elephant moja au mbili zisizo na tija kwa Taifa. Hata nchi za magharibi vyuo vya ufundi ni vingi kuliko Vyuo vikuu 4 a reason - sisi hapa kujitia wajuaji.
Uko sawa kabisa hatuwezi kuendelea bila ya kuwekeza kwenye hivi vyuo vya ufundi na Mlm.Nyerere aliliona hili, hivi vyuo ni muhimu sana pmj na Veta sasa tulipaswa tuwekeze hapa ili kwa mfano mgodi wa dhahabu kama uko Khama basi kuwe na Veta hapo hapo Kahama iliyospecialize kwenye mambo ya madini!