That's not even a question. As I said no country has been developed simply because of good or bad relationship with the west. This is to say, good relationship alone is not a [causal] factor. It depends on how you capitalize on that good relationship. North Korea is not doing fine [if they are doing fine] because of their bad relationship with the West. My problem with your [& Mwanakijiji] argument is that, you think of relationship with the west as a determining factor [ a deal breaker]. That is if you have a good relationship with the west then you should not be poor. North Korea wana uhusiano mbaya na nchi za magharibi lakini wanafanya vizuri. Sisi tuna uhusiano mzuri na nchi za magharibi lakini tunafanya vibaya. Don't you see that good relationship alone is not a factor. Now, bad relationship with the west will do more bad than good. North Korea ingekuwa wapi kama isingekuwa na vikwazo? So, maendeleo ya nchi yataletwa na wananchi wenyewe, kwa kufanya kazi. You cannot sit back and relax, ukisubiri mahusiano yetu na nchi za magharibi yawe mazuri au mabaya ndipo tuendelee. Is this what you are telling us? And why do you think you are right by suggesting that our good relationship with the west might be a reason for our mess?
Zungu, I think you misunderstand the whole sentiment behind the question; what you are saying is actually what I am implying.
Lakini pia zaidi ni kuwa Tanzania katika hali ya kawaida ingetakiwa kuwa imepiga hatua kubwa ya maendeleo kulinganisha na nchi nyingi za kiafrika au hata za mabara mengine. Hatujawahi kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, tuna mazingira mazuri ya kijiografia, kisiasa tumekuwa na utulivu wa kutosha, tuna raslimali lukuki, tuna watu wa kutosha tu kama sehemu ya nguvu kazi n.k Kwanini tupo hapa tulipo?
Kinachonogesha zaidi ni kuwa sisi ni wapokeaji wa misaada mikubwa ya kigeni wa kwanza katika Afrika (kama nchi) na kwa muda mrefu tumepokea mabilioni ya fedha za misaada na mikopo ya kila aina; zaidi ya yote tumekuwa miongoni mwa nchi zilizofutiwa karibu madeno yote yasiyolipika na nchi mbalimbali na taasisi mbalimbali za fedha. Huwezi kuelezea umaskini wetu rationally na ukaeleweka.
Katika muda wote huo ni kitu gani tumefanya ambacho kinaonesha umahiri wetu kwenye jambo lolote? Tumeunda kitu gani cha kujivunia na kusema kuwa hiki ni mazao na matunda ya ubunifu wetu? Tumeboresha kitu gani kilichoundwa na wengine na kukifanya kuwa ni cha kwetu kweli? Leo hii hata samani tunaagiza toka ng'ambo, nyanya toka ng'ambo na vitunguu toka ng'ambo. Vyote hivyo ni kwa sababu, hatuna ulazima wa kuangalia nguvu zetu wenyewe kwani kama tunaweza kuvipata kwa wenzetu why bother?
Wakati Biafra imejaribu kujitenga na Nigeria na wakawa wako under siege kwa karibu mwaka na zaidi walijikuta wanalazimika kutegemea ubunifu wao wenyewe kuendeleza viwanda, mashinde mbalimbali n.k Ni hilo hilo linalotokea Cuba na Korea ya Kaskazini. Unapojikuta umebanwa kwenye kona unalazimika kurudi kwa watu wako na uwezo wako wa ndani kuhakikisha kuwa una survive. Tanzania haijawahi kufikia mahali hapo. Kwani kwetu sisi there is no necessity!
Whatever we want our uncles can provide and whatever we short off our cousins can finance easily!
Sasa ninachojengea hoja ni kuwa kama North Korea katika kutengwa kwake na jamii ya kimataifa imefikia literacy level ya 99% wakati Tanzania ikiwa na video, na matv na ma internet bwelele level yake ni 70% then something is wrong! Kama nchi iliyotengwa na kupigwa vita na kuitwa axis of evil inaweza kutengeneza magari yake, meli zake, zana zake za kijeshi, miundo mbinu yake n.k tunaweza vipi kuelezea upungufu wetu?
Sasa sizuungumzii North Korea kama mfano wa nchi za kidemokrasia au kusema kuwa maisha ni mazuri sana na kwamba kuwa chini ya utawala wa kidikteta ni bora; ninachojengea hoja ni kuwa kuna faida gani kuishi katika uhuru na demokrasia ya vyama vingi kama muda mrefu tunatumia katika siasa, udaku, na kupiga domo!
Umesema suala ni kufanya kazi; ndiyo nakubaliana na wewe! Huko nyuma tuliwahi kuwa na "Kazii ni kipimo cha utu"; tuliukataa unyonyaji na ukabaila, tulitaka kujenga jamii ya watu wanaoheshimu na kupenda kazi. Tulianza kutengeneza vitu vyetu sisi wenyewe kwa kutumia wataalamu wetu wenyewe kuanzia radio, matairi, mashine mbalimbali, betri, zana za kilimo, n.k n.k Vyote tulivifanya kwa sababu tuliamini kuwa tunaweza kufanya mambo hayo. Wakati huo bidhaa za kigeni zilikuwa adimu na hivyo ilitulazimu kufanya mambo kivyetu vyetu.
Ndipo ikaja rukhsa!
Tukafurahia kupata mitumba sokoni, kuagiza maradio ya PANASONIG (mwenyewe nilinunua nilidhania PANASONIC!), tukafurahia kununua ma TV (nakumbuka miaka ile hadi uende Zanzibar kununua) au kwa sisi wa kanda ya ziwa kwenda Kampala! Sasa ikawa ni ruksa kubweteka kwani hatimaye vyote tunavyovitaka tunaweza kuvipata kutoka kwa "wafadhili". Matokeo yake viwanda vyetu vikaanza kufa taratibu huku tukibeza bidhaa zetu!
Na katika akili zetu wenyewe tukaamua "hey, we don't need them why don't we privatize them". tukaanza kuvigawa kama njugu na kama miogo ya kukaanga iliyowekwa masala tukaviweka juani. Aliyetaka alikuja na kutwaa kwa bei ya chee! Wenyewe tukaona sifa kuwa hatimaye tuko kwenye ubepari kweli kweli! Tukabinafsisha hadi uzalendo wetu! Katika uduni wa maoni yetu wenyewe tukaona Watanzania hawawezi kuendesha kitu chochote tukaanza kuleta wageni kutuendeshea vitu vyetu, NBC, Tanesco, ATCL, Posta n.k
Leo hii Watanzania wapo wapo tu, hata kile kidogo wanachoweza kukifanya wenyewe inabadi wapate ushauri toka kwa kina mjomba (si unakumbuka suala la Dowans na kampuni ya ushauri toka Ujerumani)?
Sasa hapa ndipo sisitunaona fahari, wakubwa wakija na kutupa pongezi tunaona sifa, matokeo yake tunalalamika kuona Wachina wanazidi kujazana na Wakenya nawatu wengine ambao wanaonekana kuchukua nafasi zetu. Really?
Sasa Korea ya Kaskazini wamelazimika kujitegemea kweli kwa karibu vitu vingi. Katika unyonge wao na katika kutengwa kwao wamelazimika kujiangalia wao wenyewe. Na katika kufanya hivyo wameweza kufanya mambo ambayo sisi wengine tunayawazia na kuombea kina Brown na Obama kutusaidia kuyafanya.
Swali linabakia, ni jinsi gani basi tunaweza kuchochea wananchi wetu kujitegemea na taifa letu kutegemea nguvu zake zenyewe, vipaji vyake na wataalamu wake? Tunaweza vipi kuamsha fikra za utafiti na ubunifu na kuzawadia vipaji mbalimbali vilivyolala ndani ya wananchi wetu? Je tuchague njia ya DPRK (piss off the West and do our own thing) au tufikiri namna mpya ya kuhusiana na nchi nyingine hasa hizi kubwa bila ya kuonekana tegemezi hadi wa fikra?