Mbalamwezi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2007
- 800
- 172
Mbalamwezi,
Lakini hatujasikia kuwa Putin amewapa Wakorea ruhusa ya kuchimba natural gas ili kugharimia huo mradi. That is the big difference! Watachimba dhahabu yetu na madini mengineyo, kugharimia mradi na faida wanaweka mfukoni.
Kwa hiyo, itakuwa vema tukiwanyima madini na tuwape mashamba pekee, tukiogopa faida watayopata kwenye madini hayo wasiweze kuwekeza shambani?
Je, ikiwa tumekubaliana nao wachimbe madini, kwa mtaji wao, nasi tukaridhika, na pia wakawekeza kwenye mashamba kwa pesa yao, iwe ya kutoka kwenye madini hayo au kwingine, tukubali?
Mimi naona tatizo si kuchimba madini au kutumia ardhi yetu, bali ni namna Tanzania inavyoweza kutajirika kutokana na mikataba tunayoingia na Wakorea.
Kwa uwezo wetu wenyewe, tumefaidikaje na ardhi kubwa hivi kama hadi leo tunalimia jembe la mkono, na hakuna hata benki moja inayomkopesha mkulima wa kawaida?
watu wetu, kwa kutokua thamani ya ardhi sasa wanawauzia wakenya, wanajenga nyumba. Kwa nini wakorea watakaowafundisha uwekezaji wa kilimo wasipangishwe ardhi, nasi tukajifunza kwao?
Hii si nchi ya kuagiza chakula na kuomba msaada wa unga toka nje, na wala si nchi ya kuingiza juisi ya matunda toka uarabuni. Lakini inafanya hivyo, kwa nini?
Kwa nini tuagize hata toothpick toka China?