Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 87
Mimi napenda sana na tena tabia ya South Korea kwa Taifa lolote lile lazima awe Mkristo hata hawa vingozi wetu ni lazima waonane kanisani ndio unaweza kupata misaada, hiyo ni HONGERA SANA kwa kazi nzuri ya kwenda huko Pinda

Bado hatujifunzi tuu? Naomba Pinda ajifunze Nicaragua jinsi wamarekani wanavyoshikilia ardhi ya nchi hiyo na namna serikali ya marekani ilivyoshiriki kupindua serikali au kuua watu walioonekana kushabikia ardhi ya kilimo cha migomba irejeshwe mikononi mwa wanicaragua. Nasi tunanaka kwenda huko?
Yaani ukitaka kujua jinsi tusivyothaminiana, hii habari mpaka itoke BBC kwanza ndiyo vyombo vya habari vya hapa nchini vihabarishwe. Kwanini kila kitu kinafanyika kisirisiri?! Hata kama mpango wote unafanyika kwa manufaa ya Watanzania, kuna ubaya gani wananchi kujulishwa wakati wa mchakato, walau kujulishwa tu viongozi wetu wamefikia wapi...
Mimi napenda sana na tena tabia ya South Korea kwa Taifa lolote lile lazima awe Mkristo hata hawa vingozi wetu ni lazima waonane kanisani ndio unaweza kupata misaada, hiyo ni HONGERA SANA kwa kazi nzuri ya kwenda huko Pinda
Katika hili kinacho takiwa kufanywa na serikali (sijui kama wamefanya hilo ni kuwapa mkataba wa miaka 50 na si zaidi) ili kama kuna uharibifu wowote basi baada ya mkataba wanaondolewa
"Some African countries export fruit and import fruit juice, or export olives and import olive oil, simply because their past colonialists did not teach them how to process food," he told the AFP news agency.
Mbalamwezi,Watanzania wengi tunatabia ya kuogopa mabadiliko. Hili ndilo linalotukwamisha sana. Katika kujadili hili, Wengine wanataka tutoe mifano ya nchi zilizofanikiwa kwa kukodisha ardhi, huku wao wakisita kutoa mifano ya nchi kama Tanzania zenye ardhi tele lakini zinanunua juisi ya embe toka Uarabuni (na hili tunaliona ni tusi, lakini kwani ni uongo jamani? Maaza zinatoka wapi? Hata Kenya tu si wananunua machungwa Muheza halafu wanatuuzia juisi?
Wengi wetu tumejadili namna tunavyoshindwa kuitumia ardhi hii kwa miaka kadhaa, lakini mbona hatuna njia mbadala za kupendekeza?
Ni kweli uongozi hauna sera makini za kutufanya tutumie ardhi kwa kutunufaisha, lakini sasa ndo tufanyeje?
Kujadili mustakabali wa taifa kwa kashfa na matusi (nasoma kuna mtu kaita mchango wa mwenzake eti "utoko," ni kielelezo cha ufinyu wa mawazo yanayotegemea kuiga tu, na wala hakuna ubunifu unaotakiwa kutuwezesha kupambana na mazingira yetu.
Tunazunguka mbuyu tu pasi na kutoa muelekeo, tutafika wapi? Ni wajibu wetu kama "great thinkers" basi kujadili hoja ya kuleta wawekezaji toka nje tukichambua kwa umahiri faida na hasara za kufanya hivyo. Katika uchumi wa sasa, kama tutaendelea kujiziba masikio na kuendelea na fikra zetu tulizodumisha kwa miaka 45 iliyopita, tutajikwamua lini na lindi hili la umasikini?
Kuna mtu ameuliza, hivi tunaweza kufanya nini kama hata kulima mpunga kwa kiwango cha kibiashara hatuwezi? poor policies, so what's next?
Nchi kadhaa zimetusaidia miradi ya kilimo iliyokufa, je, tumerithi nini toka kwa Kapunga Rice Project ya Wajapani? kuna miradi mingi ya chakula inaanzishwa na kufa mara tu wenyewe wakiondoka, je hii inatufariji sana?
Tunajisikiaje tunapoona ardhi kubwa kule Ruvu, na maji yake yanamwagika tu Baharini, wakati kuna watu wanalala njaa?
Israel ina ardhi yenye kulimika ambayo ni 2% tu ya 23,000km hivi, lakini wanajitosheleza kwa chakula na kuuza sana Ulaya. Kuna ubaya gani tukitumia ujuzi wao wa teknolojia, kwa kuchanganya na maji yetu na ardhi yetu, kujikwamua kiuchumi?
Mimi naunga mkono kuwakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kilimo cha chakula ili mradi tu maslahi ya taifa yalindwe, kuliko kuwapa wawekezaji ardhi kubwa kwa ajili ya biofuel production, ambayo ni garantii ya kutuletea mfumuko wa bei ya chakula na njaa. Mbona mnaopinga Wakorea hampingi biofuel investments ambazo ziko tayari huko bagamoyo, Kisarawe? Mnajua kuna masikini wetu sasa hawalimi mashamba yao ya mahindi na wamekimbilia kufanya kazi kwenye mashamba ya jatropha?
Mimi naona hili jambo ni sensitive sana, na tujadili kwa umakini badala ya blah blah. Hasira na kejeli haisaidii kuzuia globalisation, na hatuwezi kujifungia na ardhi yetu wakati misaada yao tunapokea kwa mikono miwili!
Dawa yake ni kujifunza namna bora zaidi ya kunufaika na ushirikiano huu wa lazima, badala ya kupiga kelele tu.
Watanzania wengi tunatabia ya kuogopa mabadiliko. Hili ndilo linalotukwamisha sana. Katika kujadili hili, Wengine wanataka tutoe mifano ya nchi zilizofanikiwa kwa kukodisha ardhi, huku wao wakisita kutoa mifano ya nchi kama Tanzania zenye ardhi tele lakini zinanunua juisi ya embe toka Uarabuni (na hili tunaliona ni tusi, lakini kwani ni uongo jamani? Maaza zinatoka wapi? Hata Kenya tu si wananunua machungwa Muheza halafu wanatuuzia juisi?
Wengi wetu tumejadili namna tunavyoshindwa kuitumia ardhi hii kwa miaka kadhaa, lakini mbona hatuna njia mbadala za kupendekeza?
Ni kweli uongozi hauna sera makini za kutufanya tutumie ardhi kwa kutunufaisha, lakini sasa ndo tufanyeje?
Kujadili mustakabali wa taifa kwa kashfa na matusi (nasoma kuna mtu kaita mchango wa mwenzake eti "utoko," ni kielelezo cha ufinyu wa mawazo yanayotegemea kuiga tu, na wala hakuna ubunifu unaotakiwa kutuwezesha kupambana na mazingira yetu.
Tunazunguka mbuyu tu pasi na kutoa muelekeo, tutafika wapi? Ni wajibu wetu kama "great thinkers" basi kujadili hoja ya kuleta wawekezaji toka nje tukichambua kwa umahiri faida na hasara za kufanya hivyo. Katika uchumi wa sasa, kama tutaendelea kujiziba masikio na kuendelea na fikra zetu tulizodumisha kwa miaka 45 iliyopita, tutajikwamua lini na lindi hili la umasikini?
Kuna mtu ameuliza, hivi tunaweza kufanya nini kama hata kulima mpunga kwa kiwango cha kibiashara hatuwezi? poor policies, so what's next?
Nchi kadhaa zimetusaidia miradi ya kilimo iliyokufa, je, tumerithi nini toka kwa Kapunga Rice Project ya Wajapani? kuna miradi mingi ya chakula inaanzishwa na kufa mara tu wenyewe wakiondoka, je hii inatufariji sana?
Tunajisikiaje tunapoona ardhi kubwa kule Ruvu, na maji yake yanamwagika tu Baharini, wakati kuna watu wanalala njaa?
Israel ina ardhi yenye kulimika ambayo ni 2% tu ya 23,000km hivi, lakini wanajitosheleza kwa chakula na kuuza sana Ulaya. Kuna ubaya gani tukitumia ujuzi wao wa teknolojia, kwa kuchanganya na maji yetu na ardhi yetu, kujikwamua kiuchumi?
Mimi naunga mkono kuwakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kilimo cha chakula ili mradi tu maslahi ya taifa yalindwe, kuliko kuwapa wawekezaji ardhi kubwa kwa ajili ya biofuel production, ambayo ni garantii ya kutuletea mfumuko wa bei ya chakula na njaa. Mbona mnaopinga Wakorea hampingi biofuel investments ambazo ziko tayari huko bagamoyo, Kisarawe? Mnajua kuna masikini wetu sasa hawalimi mashamba yao ya mahindi na wamekimbilia kufanya kazi kwenye mashamba ya jatropha?
Mimi naona hili jambo ni sensitive sana, na tujadili kwa umakini badala ya blah blah. Hasira na kejeli haisaidii kuzuia globalisation, na hatuwezi kujifungia na ardhi yetu wakati misaada yao tunapokea kwa mikono miwili!
Dawa yake ni kujifunza namna bora zaidi ya kunufaika na ushirikiano huu wa lazima, badala ya kupiga kelele tu.
Mbalamwezi,
Soma tena ripoti kwa makini. Hawa si wawekezaji. Wanakuja mkono mtupu, wachimbe madini, wakipata hela ndipo waziingize kwenye kilimo. Halafu mnagawana mavuno nusu kwa nusu wakati hela ya madini wanaweka mifukoni. Hii wala si win-win situation. Ni win situation kwa Wakorea.
Unaweza ukawa sahihi Jasusi,
lakini wanawezaje kuchimba madini wakiwa mikono mitupu, nasi tunashindwaje kuchimba madini hayo hayo mikono mitupu?