Korean Group May Build 210-Megawatt Wind Farm

Can any body come and tell us here how the electric current (or electric power) is stored after being generated? And for how long can it be stored if produced in eccess?!


Electrical enegy can not be stored but can be changed from one form of enegy to another.
 
bravo bro mwakyembe, at least hata ukiwa bilionea tuna uhakika hutatumia hizom pesa kuwanunua viongozi kama huyu mhuni wa igunga, nilikusikia ukisema kuwa ubunge siyo kazi ya kudumu, nakuaminia babake
 
This is not entirely accurate, your batteries can store electrical energy.You must be talking about AC, which does not say much about the nature of DC.

See How to Store Electricity in Batteries - Howtopedia - english

Kiranga,

I think both you and MkamaP are correct in this one. Electricity can not be stored is a correct statement, BUT, you can find a way to store electricity for example by using batteries and capacitors. In fact for a battery, what is happening is electrical energy is switched into chemical energy and back again when needed.

I can assure you if it was easy to store electricity, some of us would be importing basckets/containers full of electricity for our homes consumption.
 
Rev, Kishoka,
Umebakia pekee yako aliye muumini safi wa Ujamaa! kwi kwi kwi!
Ama kweli hawa jamaa wana kila mbinu...lakini tutafika tu..

Mtanzania,
Mkuu wait a minute... wait a minute..
yaani kweli wewe unafikiri haya maneno yana ukweli ndani yake?..
Ebu kwanza fikiria hili..
1. Week moja au mbili tu baada ya Mwakyembe kutoa taarifa yake tunaona zege hili likishindiliwa kwa haraka sana kabla ya la jana kukauka..bila kuelewa limetokea wapi..What a coincidance!

2. Msemaji mkuu ni Ngereja, waziri ambaye anawakilisha kundi la hao ma...anatutaarifu exactly kama alivyosema Mwakyembe wakati mradi huu haupo ktk miradi ya Taifa iwe kwa muda mfupi au mrefu..hakuna mwekezaji anayeweza kuwekeza ktk umeme wa Upepo toka nje kwa 100%.. hailipi hata kidogo zaidi ya kuchuma baada ya miaka 20 to 40 ktk nchi ambayo kisiasa haiko stable..nani anataka biashara kama hii?..na kibaya zaidi ni hili na tatu..
3. Mwakyembe kisha tuambia kwamba yeye alikwisha uza share zake, hivyo hana sauti wala mamlaka ya kuuza au nani apewe mradi huu kwa sababu hana share..ni mjumbe wa kamati ya nishati na madini anayetegemea kura ktk ujenzi wa policy tu, Uamuzi wa mwisho unatolewa na wizara.

Kwa hiyo tunapoambiwqa kwamba Powerpool wameuza ardhi hii inatugonganisha kimawazo kwa sababu Powerpool haikusajiliwa kama shirika la Udalali wa ardhi au Real Estate bali shirika linalofua nguvu za Umeme, mauzo ya ardhi hii yamepitishwa na nani? Na hizi taarifa za mauzo zimemfikia vipi waziri ikiwa Powerpool walikuwa hawajauza hiyo ardhi siku Mwakyembe anatoa taarifa yake..

Mkuu wangu bado mimi naamini kabisa kuwa hapa inachongwa FITNA..na kwa bahati mbaya nafikiria ujio wa hao Wakorea unaweza kumpandisha Chat mwakeyembe badala ya kumwangusha kisiasa..
Ataonekana Hero yeye kwani wadanganyika wengi hawajali zinaibiwa ngapi au at what cost ila ni kitu gani kimepatikana na nani aliyetoa Ruksa.. kumbuka utawala wa Mwinyi pamoja na madudu yote ya Kiuchumi ndiye rais anayependwa kuliko wote kwa sababu ya RUKSA!...

Pamoja na yote haya kama kweli Mwakyembe yuko nyuma ya uuzaji wa ardhi hiyo kwa hawa Wakorea.. basi mkuu wangu nimechoka lakini kama hawa jamaa ni wajenzi tu na Powerpool ndiye mmliki wa nguvu hizi za Umeme basi hapa nawapa pongezi viongozi wote wa shirika hili la wananchi wazalendo, wazawa...
 


Mkandara,

Aliziuza wapi hizo shares? Mbona ukisoma alichoongelea kwenye suala zima inaonekana ana jikanganya mwenyewe na kuzunguka mbuyu? Mara ana uchungu, mara yeye na washirika wake ni masikini, mara umeme huu utalisaidia Taifa, lakini katika press release sikumbuki kusoma akisema alishauza hizo sharesa!

Kama aliuza, labda nimuulize, kwa nini aliuza shares za mradi mkubwa kama huo? what happened?
 

Those baskets are otherwise known as batteries, as you aptly noted
 
Mkuu Mkandara,

Ukiuza shares Tanzania unalipa TRA na kupewa receipt. Ungelikuwa wewe si ungeitanguliza hiyo receipt ili kila mtu ajue umeuza? Kwa jinsi nilivyosikiliza mimi, nakubaliana na Rev. Kishoka hakusema waziwazi kwamba ameuza.

Nafikiri imetokea coincidence haya mambo yote yamekuja kwa wakati mmoja. Hivi Zanzibar kulikuwa na mkutano wa wawekezaji wiki hii? Maana nimeona habari mbalimbali za biashara zinatangazwa tokea Zanzibar ikiwemo ile ya TBL.

Hii habari hata mimi imenichanganya. Ila kama ni kweli basi nitaona wahusika kumbe sio makini kabisa. Haiwezekani ukawa unatetea huo mradi kwa kisingizio cha uzawa huku mkono mwingine unauza kwa wageni. Labda hawa Wakorea wamedanganya na hawajauziwa huo mradi.

Wakati Dr anaongea kuna mambo ambayo mimi nilishika kichwa. Kwa mfano alipotaja hizo 1800 Megawatt. Wakorea waliporudia hiyo namba ndio nikajua nini kinaendelea.
 
Electrical enegy can not be stored but can be changed from one form of enegy to another.

Do you mean it can be stored after changing it into another form of energy??!! And what is that form of energy which can be stored?!
 
Last edited:

Does it mean that electric energy produced at KIDATU for instance is transported (distributed) to end user(consumer) immediately after being generated??!!
 
This is not entirely accurate, your batteries can store electrical energy.You must be talking about AC, which does not say much about the nature of DC.

See How to Store Electricity in Batteries - Howtopedia - english

thank you very much.

Electrical energy can not be stored BUT Electrical charges can be stored or created and what is Energy ? Is the one which cause charges move from valence band to conduction band .Any charge in conduction band is set free to move and the rate of charge or the number of charges which will flow under a given fixed time of observation is what termed current and the robot aka energy which cause charges move also is termed voltage.
 
Last edited:
Does it mean that electric energy produced at KIDATU for instance is transported (distributed) to end user(consumer) immediately after being generated??!!



YES inaingizwa moja kwa moja kwenye line
lakini kwa sababu ya cases za loss of energy inayotokana na transportation ndio inapitishwa ktk step up then step down transfoma.
 
Rev, Kishoka,
Mkuu hukufuatilia Invinsible alipokuwa akitupa dondoo za mkutano wa Mwakyembe na waandishi wa habari?..
Kuna sehemu mbili moja Invincible alimnukuu Mwakyembe akisema:-
1. Mwakyembe anadai Alishaondoka kwenye kampuni hiyo na wanaopinga wafuatilie updates za Brela za 2006/07.
Manyerere bado yupo Habari Corporation (alirudi) hii ipo page two..

Bila shaka ktk Private company huwezi kudai umeondoka kama bado una shares.. unaweza kuwa dormant lakini sio kuondoka..

2. Wakuu kifupi Mwakyembe amesema YEYE alishajiondoa kwenye kampuni kama mwana hisa lakini yeye pamoja na wabunge wengi wanaiunga mkono kampuni hii na wanaendelea mpaka sasa kuwa interested nayo kwani ni ya wazalendo na haijawahi kupata mkopo toka benki yoyote japo ni ya wazawa (page three)..


Sasa tukitazama habari za huyu Mkorea mwenyewe hatupati jibu wazi! Hilo shirika la Good PM group nalo linaonekana kama kanyanga tu!..nashindwa kuoanisha habari hii na ukweli zaidi ya kuwa maneno haya yamepikwa na kuwekwa mdomoni mwa Mkorea mmoja lifemember wa Jolly Club, hao wanaokuja kuuza tiles nchini na kurudi kwao na vito vya Tanzanite..

Yawezekana kweli hii project ipo kama ilivyodaiwa lakini nashindwa kuelewa hiyo memorandum of understanding inasema nini!..kweli wamenunua, Na imekuwaje tunaona kuwa hao hao Wakorea wakizungumziwa kama investors halafu tena ni contractors wakitumia wingi wa group of Koreans mara P.M group...Yaani balaa tupu ukichanganya na moto wa Mwakyembe..

Hapa mkuu wangu ni changa la macho tu..
 

Wakuu Mkandara & Kishoka,

Tusichanganywe na hawa akina Ngeleja. Sidhani hao Wakorea ndio hao hao Power Pool.

Ngeleja amewekwa pale kufanikisha mambo ya Lowassa na RA. Nia yao kubwa ni kubwa ni kumiliki uzalishaji wa umeme Tanzania na ndio maana wamepanga watu wao kuanzia Wizara ya Nishati na Madini mpaka Tanesco.

Nina uhakika baada ya kuona Mwakyembe amelipigia debe hili la wind power kuwa na wananchi wengi kulipa kudo kuwa ni zuri kwa maslahi ya Taifa, basi hapo ndio na hawa makuwadi walipoamua kumtuma Ngeleja kutueleza kuwa kuna Wakorea watakaokuja kutuwekea wind mills.

Ukweli hapa ni kuwa hawa ni wale wale Richmond=Dowans=Wakorea.

Tung'ang'anie kupata data za hiyo kampuni ya Wakorea ili tuipambanue.
 
Kwa nini Serikali isitumie pesa ya kodi ..waweke ktk budget ya 2009/10... 500 Billion kuanzisha miradi mikubwa kama hii??

Watu watasema budget kidogo hapana.. wapunguze matumizi na kupunguza wizara, na posho na safari za ajabu ajabu!

Au serikali ichukue mkopo mkubwa toka IMF, WB, Saudia, Norway au China wa 1 billion USD and invest ktk miradi mikubwa?

Why serikali inakuwa na fire brigade measures kama za Richmond?
 
....tatizo ni policy za umeme ambazo zinatakiwa kubadilishwa,ruhusu watu binafsi wazalishe na kuuza umeme moja kwa moja kwa wananchi kuliko kuwabana bana lazima wauzie TANESCO...mafisadi na TANESCO ndio wanajipatia sehemu ya kura hapo na rushwa zote ni hapo hapo kwenye kuuziana huo umeme,huu upuuzi lazima uishe la sivyo hakuna serious investor anaweza kuweka pesa zake kwenye miradi ambayo faida yako inategemea uwahonge mafisadi!
 
Wakuu Mkandara & Kishoka,

Tusichanganywe na hawa akina Ngeleja. Sidhani hao Wakorea ndio hao hao Power Pool.



Makaayamawe,

Uko serious kwamba tunaongelea kampuni mbili tofauti?

Kama ulisoma maelezo ya Tanesco, waziri Ngeleja, Dr. Mwakyembe na sasa Mkorea, wote wanaongelea umeme wa upepo Singida na kuanza 2011.

Figures mbalimbali za Dr. Mwakyembe zinafanana kabisa na za huyu Mkorea ikiwemo ya megawatt 1800.

Inaelekea hili suala linajulikana siku nyingi kwenye sector ya nishati. Kama umefuatilia, Shelukindo katoa na siri ambayo tulikuwa hatuijui, kwamba hawa jamaa na kampuni yao mpaka tayari walishafika na kwenye kamati ya nishati na madini.

Mkorea kamalizia kabisa na kwa kuwataja waliowauzia ardhi, ni kampuni ile ile ambayo documents zake tunazo hapa ya Power Pool East Africa Ltd.

Tuone kama waheshimiwa watakuja kukanusha tena.
 

Kifupi ni ile ile na eneo ni lilelile hao ndio wawekezaji wazalendo,kwa maoni yangu akina Mwakyembe wamewahadaa wananchi wa singida yani wamewapiga changa la macho wakapewa bure ama kwa fedha kidogo wakijiita wazalendo harafu ardhi hiyohiyo wanaiuza kwa bei ya juuuuuuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…