Rev, Kishoka,
Umebakia pekee yako aliye muumini safi wa Ujamaa! kwi kwi kwi!
Ama kweli hawa jamaa wana kila mbinu...lakini tutafika tu..
Mtanzania,
Mkuu wait a minute... wait a minute..
yaani kweli wewe unafikiri haya maneno yana ukweli ndani yake?..
Ebu kwanza fikiria hili..
1. Week moja au mbili tu baada ya Mwakyembe kutoa taarifa yake tunaona zege hili likishindiliwa kwa haraka sana kabla ya la jana kukauka..bila kuelewa limetokea wapi..What a coincidance!
2. Msemaji mkuu ni Ngereja, waziri ambaye anawakilisha kundi la hao ma...anatutaarifu exactly kama alivyosema Mwakyembe wakati mradi huu haupo ktk miradi ya Taifa iwe kwa muda mfupi au mrefu..hakuna mwekezaji anayeweza kuwekeza ktk umeme wa Upepo toka nje kwa 100%.. hailipi hata kidogo zaidi ya kuchuma baada ya miaka 20 to 40 ktk nchi ambayo kisiasa haiko stable..nani anataka biashara kama hii?..na kibaya zaidi ni hili na tatu..
3. Mwakyembe kisha tuambia kwamba yeye alikwisha uza share zake, hivyo hana sauti wala mamlaka ya kuuza au nani apewe mradi huu kwa sababu hana share..ni mjumbe wa kamati ya nishati na madini anayetegemea kura ktk ujenzi wa policy tu, Uamuzi wa mwisho unatolewa na wizara.
Kwa hiyo tunapoambiwqa kwamba Powerpool wameuza ardhi hii inatugonganisha kimawazo kwa sababu Powerpool haikusajiliwa kama shirika la Udalali wa ardhi au Real Estate bali shirika linalofua nguvu za Umeme, mauzo ya ardhi hii yamepitishwa na nani? Na hizi taarifa za mauzo zimemfikia vipi waziri ikiwa Powerpool walikuwa hawajauza hiyo ardhi siku Mwakyembe anatoa taarifa yake..
Mkuu wangu bado mimi naamini kabisa kuwa hapa inachongwa FITNA..na kwa bahati mbaya nafikiria ujio wa hao Wakorea unaweza kumpandisha Chat mwakeyembe badala ya kumwangusha kisiasa..
Ataonekana Hero yeye kwani wadanganyika wengi hawajali zinaibiwa ngapi au at what cost ila ni kitu gani kimepatikana na nani aliyetoa Ruksa.. kumbuka utawala wa Mwinyi pamoja na madudu yote ya Kiuchumi ndiye rais anayependwa kuliko wote kwa sababu ya RUKSA!...
Pamoja na yote haya kama kweli Mwakyembe yuko nyuma ya uuzaji wa ardhi hiyo kwa hawa Wakorea.. basi mkuu wangu nimechoka lakini kama hawa jamaa ni wajenzi tu na Powerpool ndiye mmliki wa nguvu hizi za Umeme basi hapa nawapa pongezi viongozi wote wa shirika hili la wananchi wazalendo, wazawa...