Nakumbuka maisha ya zamani, sasa Nimeanza kupita mjini kuulizia bei ya koroboi na mafuta ya taa kwani umeme huu haueleweki kabisa. Sijaona koroboi mjini Dar, labda nitoe nitengeneze mwenyewe na kusokota utambi wa kanga na kuweka mafuta ya taa. Sina shida na umeme tena.
Naona wewe ni mtaalamu kweli. Kwa watanzania wengi walio vijijini wanatumia kibatari au koroboi. Twaweza kurudi huko km mambo ya umeme yataendelea namna hii.
Yaoneka mh hujaishi maisha haya. Tulitumia kila siku na hatukupata mafua. Mpaka leo hii wanaoishi miaka mingi ni walio vijijini, na ndio wanaotumia koroboi.