kabanga
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 37,421
- 18,760
Wanasayansia nchini Marekani wamefaulu katika kuunda korodani za bandia ambazo zinao uwezo mkubwa wa kuzalisha shahawa kwa wanaume wagumba.
Kifaa hicho kitamsaidia mwanaume asiye na uwezo wa kutungisha mimba, kuweza kutungisha mimba kwa mwenza wake kama wanaume wengine.
Ni kama mashine ya kuzalisha shahawa, anasema Dk Paul Turek, Mkurugenzi wa Kliniki ya Turek, ambayo imejikita katika masuala ya ugumba kwa wanaume.
Dk Turek anasema hawatapandikiza korodani kwa mwanaume, bali wataunda mashine ya kibaolojia ya kuzalisha shahawa ambayo itawasaidia hata wanasayansi kujifunza zaidi chanzo cha ugumba kwa wanaume.
Daktari huyo anasema kuunda korodani si kazi rahisi, lakini watatumia taratibu kadhaa za kimaabara ambazo zitaunda korodani inayoweza kuzalisha shahawa kama korodani halisi.
Kwanza, tutaunda seli ambazo zitakuza shahawa ndani ya maabara kisha tutaongeza seli za mwanadamu ambazo zikiungana zitaunda seli mpya anasema
Nchini Tanzania, Daktari wa Masuala ya Mfumo wa Mikojo kwa Wanaume na Wanawake na Uzazi kwa Wanaume,(Urology), Profesa Sydney Yongolo wa Hospitali ya Tumaini anakubali kuwapo kwa uwezekano wa korodani kuundwa maabara kwani siku hizi wanasayansi wana uwezo wa kuunda kila kitu, ili mradi tu wapate fedha za utafiti.
Anasema hapo zamani ilikuwa vigumu kwa wanasayansi kuunda ogani za mwili wa mwanadamu, lakini hivi karibuni kibofu cha mkojo kimetengenezwa maabara na kinafanya kazi na hivi karibuni wanasayansi wamejaribu pia kuunda figo ambayo imefanya kazi kwa panya.
Anasema kuundwa kwa korodani bandia ni jambo linalowezekana kwa wanasayansi wanaotumia muda wao vyema katika tafiti za kisayansi.
Dk Turek anasema kwa kawaida seli ndani ya korodani hupitia harua 12 hadi kufikia kuwa shahawa kamili hivyo korodani ya bandia itasadifu mchakato wote huo.
Korodani hiyo itatengenezewa mazingira kama yale yaliyoko katika korodani halisi ili kuwezesha shahawa kusafiri na kuingia katika uke.