Korogwe: Mamlaka ondoeni barabarani masalia ya mwili wa marehemu aliyegongwa na lori la mchanga

Korogwe: Mamlaka ondoeni barabarani masalia ya mwili wa marehemu aliyegongwa na lori la mchanga

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Tarehe 23/1/2022 majira ya saa 1 usiku kuna kijana wa bodaboda aligongwa na Isuzu Tipper barabara kuu ya Moshi Dsm eneo la Mwembeni na kufariki papo hapo.

Marehemu alijeruhiwa kichwani na kumwaga ubongo wote barabarani. Mpaka leo 26/1/2022 bado kuna masalia mengi ya ubongo na nywele za marehemu.

Hata ukipita kwenye basi unaona kabisa.

Ni huzuni kubwa sana (RIP).

Halmashauri ya Mji Korogwe ina Mamlaka zinazoweza kutoa uchafu ule pale barabarani. Wana kampuni za kufanya usafi Mjini n.k.

Tumheshimu marehemu aisee.
 
Unauita ubongo wa mtu uchafu?
Uchafu Ni nini mkuu? Uchafu ni kitu chochote kukaa mahali ambapo hapastahili kitu hicho kuwa pale.

Hata nguo yako unayoipenda Sana ukiiweka mahali ambapo si mahali pake Basi huo ni uchafu,kinyesi kinapokuwa chooni huwezi kukiita ni uchafu maana chooni ni mahali pake,ikiwa kinyume chake Basi huo ni uchafu
 
Upo sahihi ila sasa haijakaa sawa sana katika hayo mazingira kusema hivyo.

Ukitaka kuamini ule uwe ubongo wa mtu wako wa karibu halafu unamsikia mwingine akisema hivyo.
 
Hivi Kunguru wa Korogwe wako likizo?

Mbona hapa Temeke Bodaboda akimwaga Ubongo Kunguru wa Dar wanasafisha mara moja.
 
Unauita ubongo wa mtu uchafu?

Upo sahihi ila sasa haijakaa sawa sana katika hayo mazingira kusema hivyo.

Ukitaka kuamini ule uwe ubongo wa mtu wako wa karibu halafu unamsikia mwingine akisema hivyo.

asante kwa taarifa lakini hauna busara.

Ungekuwa ubongo wako nao ungeitwa uchafu

Umetoa hoja nzuri mwishoni umeharibu mkuu

Ukifa basi tungeita mzoga ndio maana hata mwili uokotwe mtoni huwezi kuita mizoga au neno lolote baya

Tafsida ikusaidie boss
Ni uchafu tu haijalishi ungekuwa barababrani au mochwari au kaburini. Binadamu ukishakufa hauna thamani tena, msijifariji kijinga.
 
masalia ya mwili wa marehem.ndo lugha nzuri mkuu.ila Asante kwa kuwakumbusha wahusika.
 
Dah inasikitisha na inasikitisha zaidi kuita ubongo wa mwanadamu aliyetangulia sote tuendako uchafu
 
Halafu hilo eneo halijakaa vizuri hata kidogo kutokana na msongamano wa watu, bajaj, bodaboda, magari, nk! Ni vizuri yakawekwa matuta.

Ingawa bodaboda nao ifikie wakati waendeshe pikipiki zao huku wakichukua tahadhari! Tabia ya kuingi tu barabara kuu kiholela, ni hatari sana kwa usalama wao.
 
Mkuu huyo boda boda aliegongwa aitwa Nani pengine anaweza kua alikua jamaa yangu.Na ni mwembeni Kama waelekea upande upi? Shell au bank?
 
Back
Top Bottom